Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 18:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 “Mtakapofika katika ile nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawapa, msifuate desturi za kuchukiza za mataifa hayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 “Mtakapofika katika ile nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawapa, msifuate desturi za kuchukiza za mataifa hayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 “Mtakapofika katika ile nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawapa, msifuate desturi za kuchukiza za mataifa hayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Mtakapoingia katika nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapa, msijifunze kuiga njia za machukizo za mataifa ya huko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Wakati mtakapoingia katika nchi ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa, msijifunze kuiga njia za machukizo za mataifa ya huko.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 18:9
11 Marejeleo ya Msalaba  

wakafukiza uvumba huko katika kila mahali pa juu, kama mataifa walivyofanya, ambao BWANA aliwafukuza mbele yao; wakaunda mambo mabaya, ili wamkasirishe BWANA;


Wakaziendea sheria za mataifa, ambao BWANA aliwafukuza mbele ya wana wa Israeli, na sheria za wafalme wa Israeli walizozifanya.


Tena akafukiza uvumba katika bonde la mwana wa Hinomu, akawateketeza wanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli.


Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno wakifuata machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA aliyoitakasa katika Yerusalemu.


BWANA asema hivi, Msijifunze njia ya mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara za mbinguni; maana mataifa hushangaa kwa sababu ya ishara hizo.


Kwa hiyo yafuateni maagizo yangu, ili kamwe msiwe na mojawapo ya tabia hizi zinazochukiza, zilizotangulia kufanywa mbele zenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


wasije wakawafunza kufanya mfano wa machukizo yao yote, waliyoifanyia miungu yao; hivyo itakuwa ni makosa juu ya BWANA, Mungu wenu.


Usiseme moyoni mwako, BWANA, Mungu wako, atakapokwisha kuwasukumia nje mbele yako, ukasema, Ni kwa haki yangu alivyonitia BWANA niimiliki nchi hii; kwani ni kwa ajili ya uovu wa mataifa haya BWANA anawafukuza nje mbele yako.


Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya BWANA, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno BWANA alilowaapia baba zako Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo