Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 18:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Kwani BWANA, Mungu wako, amemchagua katika kabila zako zote, asimame atumike kwa jina la BWANA, yeye na wanawe milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Katika makabila yenu yote, Mwenyezi-Mungu amechagua kabila la Walawi limtumikie kama makuhani milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Katika makabila yenu yote, Mwenyezi-Mungu amechagua kabila la Walawi limtumikie kama makuhani milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Katika makabila yenu yote, Mwenyezi-Mungu amechagua kabila la Walawi limtumikie kama makuhani milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewachagua pamoja na wazao wao kutoka makabila yenu kusimama na kuhudumu katika jina la Mwenyezi Mungu siku zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu wenu amewachagua pamoja na wazao wao kutoka makabila yenu kusimama na kuhudumu katika jina la bwana siku zote.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 18:5
9 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe, na kuwavika kofia; nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele; nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.


kisha akanena na Kora na mkutano wake wote, akawaambia, Asubuhi BWANA ataonesha ni kina nani walio wake, kisha ni nani aliye mtakatifu, tena ni nani atakayemkaribisha kwake; maana, yeye atakayemchagua ndiye atakayemsongeza kwake.


tena kwake yeye, na kizazi chake baada yake, litakuwa agano la ukuhani wa milele; kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu wake, na kuwafanyia upatanisho wana wa Israeli.


Nawe utawaweka Haruni na wanawe, nao wataushika ukuhani wao, na mgeni atakayekaribia atauawa.


Na wakati huo BWANA alilitenga kabila la Lawi ili walichukue lile sanduku la Agano la BWANA, wasimame mbele ya BWANA kwa kumtumikia, na kuwabarikia watu kwa jina lake, hata hivi leo.


Na mtu afanyaye kwa kujikinai, kwa kutomsikiza kuhani asimamaye hapo kwa kumtumikia BWANA, Mungu wako, au mwamuzi, na afe mtu huyo; nawe utauondoa uovu katika Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo