Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 18:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 wala mchawi, wala mlozi, wala mwenye kutaka kauli kwa mizimu na pepo au kutoka kwa wafu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 wala mchawi, wala mlozi, wala mwenye kutaka kauli kwa mizimu na pepo au kutoka kwa wafu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 wala mchawi, wala mlozi, wala mwenye kutaka kauli kwa mizimu na pepo au kutoka kwa wafu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 wala arogaye kwa kupiga mafundo, wala mwaguzi au anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 wala arogaye kwa kupiga mafundo, wala mwaguzi au anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 18:11
9 Marejeleo ya Msalaba  

Usimwache mwanamke mchawi kuishi.


Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?


Msile kitu chochote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.


Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


Tena mwanamume au mwanamke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.


Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.


Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, tulikutana na kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi, aliyewapatia bwana zake faida kubwa kwa kuagua.


Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye pamoja na watu wawili wakamfikia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukaniletee yeye nitakayemtaja kwako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo