Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 17:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa BWANA amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Hata hivyo, asiwe na farasi wengi kwa ajili yake mwenyewe, wala asiwarudishe watu Misri ili kujipatia farasi zaidi, kwa kuwa Mwenyezi-Mungu amewaonya, ‘Kamwe msirudi huko tena’.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Hata hivyo, asiwe na farasi wengi kwa ajili yake mwenyewe, wala asiwarudishe watu Misri ili kujipatia farasi zaidi, kwa kuwa Mwenyezi-Mungu amewaonya, ‘Kamwe msirudi huko tena’.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Hata hivyo, asiwe na farasi wengi kwa ajili yake mwenyewe, wala asiwarudishe watu Misri ili kujipatia farasi zaidi, kwa kuwa Mwenyezi-Mungu amewaonya, ‘Kamwe msirudi huko tena’.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Hata hivyo, kamwe mfalme asijipatie hesabu kubwa ya farasi kwa ajili yake mwenyewe, au kuwafanya watu warudi Misri ili kupata farasi wengi, kwa maana Mwenyezi Mungu amekuambia, “Hamtairudia njia ile tena.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Hata hivyo, kamwe mfalme asijipatie hesabu kubwa ya farasi kwa ajili yake mwenyewe, au kuwafanya watu warudi Misri ili kupata farasi zaidi, kwa maana bwana amekuambia, “Hamtairudia njia ile tena.”

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 17:16
23 Marejeleo ya Msalaba  

Daudi akampokonya wapanda farasi elfu moja na mia saba na askari waliokwenda kwa miguu elfu ishirini; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila farasi wa magari mia moja akawabakiza.


Ndipo Adonia mwana wa Hagithi akatakabari, akasema, Mimi nitakuwa mfalme. Akajiwekea tayari magari na wapanda farasi, na watu hamsini wapige mbio mbele yake.


Tena Sulemani alikuwa na mabanda ya farasi elfu arubaini kwa magari yake, na wapandao farasi elfu kumi na mbili.


Basi uamuru wanikatie mierezi ya Lebanoni; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni.


Nao farasi, aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi; kila kundi na thamani yake.


Sulemani akawa na mazizi ya farasi na magari elfu nne, na wapandao farasi elfu kumi na mbili, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu.


Hawa wanataja magari na hawa farasi, Lakini sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.


Ilikuwa hapo Farao alipowaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakabadili nia watu hawa hapo watakapokumbana na vita, na kurudi Misri;


lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri wakiwa tayari kwa vita.


Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.


Tena nchi yao imejaa fedha na dhahabu, wala hapana mwisho wa hazina zao; tena nchi yao imejaa farasi, wala hapana mwisho wa magari yao.


BWANA asema katika habari zenu, enyi mabaki ya Yuda, Msiingie Misri; jueni sana ya kuwa nimewashuhudia hivi leo.


Lakini alimwasi kwa kutuma wajumbe huko Misri, wampe farasi na watu wengi. Je! Atafanikiwa? Afanyaye mambo hayo ataokoka? Atalivunja agano, kisha akaokoka?


Hatarudi tena nchi ya Misri; bali huyo Mwashuri atakuwa mfalme wake; kwa sababu walikataa kurejea.


Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema.


Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema BWANA, nitawakatilia mbali farasi wako watoke kati yako, nami nitayaharibu magari yako ya vita;


BWANA atakurudisha tena Misri kwa merikebu, kwa njia ambayo nilikuambia, Hutaiona tena popote; nanyi huko mtajiuza nafsi zenu kwa adui zenu kuwa watumwa na wajakazi, wala hapana atakayewanunua.


Akasema, Mfalme atakayewatawala ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, katika magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo