Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 17:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 usiache kumweka yule atakayechaguliwa na BWANA, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye si ndugu yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 mwaweza kumweka mfalme juu yenu mtu ambaye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atamchagua. Mtamweka mmojawapo wa ndugu zenu kuwa mfalme juu yenu. Msimfanye mgeni asiye ndugu yenu kuwa mfalme wenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 mwaweza kumweka mfalme juu yenu mtu ambaye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atamchagua. Mtamweka mmojawapo wa ndugu zenu kuwa mfalme juu yenu. Msimfanye mgeni asiye ndugu yenu kuwa mfalme wenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 mwaweza kumweka mfalme juu yenu mtu ambaye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atamchagua. Mtamweka mmojawapo wa ndugu zenu kuwa mfalme juu yenu. Msimfanye mgeni asiye ndugu yenu kuwa mfalme wenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 kuweni na uhakika wa kumweka mfalme juu yenu ambaye Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atamchagua. Ni lazima atoke miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msimweke mgeni juu yenu ambaye si ndugu Mwisraeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 kuweni na uhakika wa kumweka mfalme juu yenu ambaye bwana Mwenyezi Mungu wenu atamchagua. Ni lazima atoke miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msimweke mgeni juu yenu ambaye si ndugu wa Kiisraeli.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 17:15
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo watu wa kabila zote za Israeli wakamwendea Daudi huko Hebroni, wakasema naye, wakinena, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako.


Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli wakitoka nje kwenda, na kurudi vitani. Naye BWANA akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya Israeli.


Na hizi ni hesabu za vichwa vya watu wenye silaha za vita, waliokuja Hebroni kwa Daudi, ili kumpa ufalme wa Sauli, sawasawa na neno la BWANA.


huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu; naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa babaye; nami nitakiimarisha milele kiti cha ufalme wake juu ya Israeli.


tena katika wana wangu wote (kwani BWANA amenipa wana wengi), amemchagua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA, juu ya Israeli.


Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,


Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.


Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu.


Zuia mguu wako usikose kiatu, na koo yako isiwe na kiu; lakini wewe ulisema, Hakuna matumaini kabisa; la, maana nimewapenda wageni, nami nitawafuata.


Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; nami nitamkaribisha, naye atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu kunikaribia? Asema BWANA.


Basi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, ama sivyo?


Samweli akawaambia watu wote, Mnamwona mtu huyu aliyechaguliwa na BWANA, kwamba hakuna mtu mfano wake katika watu wote. Ndipo watu wote wakapiga kelele, wakasema, Mfalme na aishi!


Umwalike Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonesha utakayotenda; nawe utampaka mafuta yule nitakayemtaja kwako.


wakamwambia, Angalia, wewe umezeeka, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tuteulie mfalme atutawale kama mataifa yale mengine yote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo