Kumbukumbu la Torati 17:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC
11 kwa mfano wa sheria watakayokufunza, na kwa mfano wa hukumu watakayokuambia, fanya vivyo hivyo; usigeuke katika hukumu watakayokuonesha, kwenda mkono wa kulia wala wa kushoto.
Mfalme akasema, Je! Si mkono wa Yoabu ulio pamoja nawe katika haya yote? Mwanamke akajibu, akasema, Kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mfalme, hapana mtu awezaye kugeuka kwa kulia, au kwa kushoto, kukana neno lolote alilolisema bwana wangu mfalme; kwani mtumishi wako Yoabu ndiye aliyeniamuru, na kuyaweka maneno haya yote kinywani mwa mjakazi wako;
moyo wake usije ukainuliwa juu ya ndugu zake, wala asikengeuke katika maagizo, kwa mkono wa kulia wala wa kushoto; ili apate kuzifanya siku zake kuwa nyingi katika ufalme wake, yeye na wanawe, katikati ya Israeli.
Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda kulingana na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kulia, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.
Basi, iweni thabiti sana kuyashika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati ya Musa, na kuyatenda, msiyaache kwa kugeukia upande wa kulia wala upande wa kushoto.