Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 16:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Nawe umchinjie Pasaka BWANA, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Mtatoa sadaka ya Pasaka kutoka mifugo yenu ya kondoo au ng'ombe kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atachagua likae jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Mtatoa sadaka ya Pasaka kutoka mifugo yenu ya kondoo au ng'ombe kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atachagua likae jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Mtatoa sadaka ya Pasaka kutoka mifugo yenu ya kondoo au ng'ombe kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atachagua likae jina lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo, au la ng’ombe, mahali atakapopachagua Mwenyezi Mungu kuwa makao kwa ajili ya Jina lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo au la ng’ombe, mahali pale ambapo bwana atapachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 16:2
19 Marejeleo ya Msalaba  

Naye mfalme akawaamuru watu wote, akasema, Mfanyieni BWANA, Mungu wenu, Pasaka, kama ilivyoandikwa katika kitabu hiki cha agano.


Tena Yosia akawapa watu, matoleo ya makundi, wana-kondoo na wana-mbuzi, yote yawe kwa ajili ya matoleo ya Pasaka, wote waliokuwako, wakiwa elfu thelathini, na ng'ombe elfu tatu; hao walitoka katika mali za mfalme.


Tena, wana wa Israeli na waadhimishe sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa.


Katika siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Ni wapi utakapo tukuandalie uile Pasaka?


Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa asulubiwe.


Katika siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja Pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile Pasaka?


Akawaambia, Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu;


Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie Pasaka tupate kuila.


Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;


wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.


bali katika mahali atakapopachagua BWANA katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote ninayokuamuru.


lakini hivyo mtakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, wewe, na mwanao wa kiume na wa kike, na mtumwa wako mume na mke, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako.


Ila vitu vyako vitakatifu ulivyo navyo, na nadhiri zako, uvitwae uende mahali atakapochagua BWANA;


Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika makabila yenu yote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe uende huko;


Utamla mbele za BWANA, Mungu wako, mwaka hata mwaka mahali atakapochagua BWANA, wewe na nyumba yako.


Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie Pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako.


Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba utakula naye mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoka nchi ya Misri, siku zote za maisha yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo