Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 16:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Kila mtu na atoe kama awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya BWANA, Mungu wako, alivyokupa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Wote watatoa kadiri wanavyoweza kulingana na baraka Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alizowajalia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Wote watatoa kadiri wanavyoweza kulingana na baraka Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alizowajalia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Wote watatoa kadiri wanavyoweza kulingana na baraka Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alizowajalia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kila mmoja wenu ni lazima alete zawadi kulingana na jinsi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alivyowabariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kila mmoja wenu ni lazima alete zawadi kulingana na jinsi ambavyo bwana Mwenyezi Mungu wenu alivyowabariki.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 16:17
10 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.


Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.


Naye atatengeneza sadaka ya unga, efa moja kwa ng'ombe dume, na efa moja kwa kondoo dume, na kwa wale wana-kondoo, kwa kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta kwa efa moja.


Lakini akiwa ni maskini zaidi ya kuhesabu kwako, ndipo atawekwa mbele ya kuhani, na huyo kuhani atamkadiria; kama uwezo wake huyo aliyeweka nadhiri ulivyo, ndivyo kuhani atakavyomkadiria.


Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.


Nawe sikukuu ya majuma umfanyie BWANA, Mungu wako, kwa kutoa sadaka ya hiari ya mkono wako, utakayotoa kwa kadiri akubarikiavyo BWANA, Mungu wako;


Mara tatu kwa mwaka na watokee wana wa kiume wako wote mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua; katika sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, na katika sikukuu ya majuma, na katika sikukuu ya vibanda; wala wasitokee mbele za BWANA mikono mitupu.


Weka waamuzi na maofisa katika malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako; nao wawaamue watu kwa maamuzi ya haki.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo