Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 16:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Siku saba mfanyie sikukuu BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, atakubariki katika mavuno yako yote, na katika kazi zote za mikono yako, nawe uwe katika kufurahi kabisa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Kwa siku saba mtamfanyia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, sherehe mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atapachagua; kwa sababu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki kwa mazao yenu yote na katika shughuli zenu zote nanyi hakika mtafurahi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Kwa siku saba mtamfanyia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, sherehe mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atapachagua; kwa sababu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki kwa mazao yenu yote na katika shughuli zenu zote nanyi hakika mtafurahi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Kwa siku saba mtamfanyia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, sherehe mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atapachagua; kwa sababu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki kwa mazao yenu yote na katika shughuli zenu zote nanyi hakika mtafurahi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, katika mahali atakapopachagua Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu ya bwana Mwenyezi Mungu wenu katika mahali atakapopachagua bwana. Kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu wenu atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 16:15
11 Marejeleo ya Msalaba  

Na mkutano wote wa watu, waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, wakatengeneza vibanda, wakakaa katika vibanda hivyo; maana tangu siku za Yoshua, mwana wa Nuni, hadi siku ile, wana wa Israeli hawakufanya hivyo. Pakawa na furaha kubwa sana.


siku ambazo Wayahudi walijipatia raha mbele ya adui zao, na mwezi uliogeuzwa kwao kuwa furaha badala ya huzuni, na kuwa sikukuu badala ya kilio; wazifanye siku hizo ziwe za karamu na furaha, za kupeana zawadi na za kuwapa maskini tunu.


Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika makabila yenu yote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe uende huko;


Nawe sikukuu ya majuma umfanyie BWANA, Mungu wako, kwa kutoa sadaka ya hiari ya mkono wako, utakayotoa kwa kadiri akubarikiavyo BWANA, Mungu wako;


nawe utafurahi katika sikukuu yako, wewe, na mwanao, na binti yako, na mtumwa wako, na mjakazi wako, na Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako.


Mara tatu kwa mwaka na watokee wana wa kiume wako wote mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua; katika sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, na katika sikukuu ya majuma, na katika sikukuu ya vibanda; wala wasitokee mbele za BWANA mikono mitupu.


kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda BWANA, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.


naye atakupenda na kukubariki na kukuongeza tena ataubariki uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, kuongezeka kwa ng'ombe na kondoo wako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo