Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 15:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; jicho lako likawa ovu juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Angalieni wazo ovu lisiwaingie mioyoni mwenu, mkasema: ‘Mwaka wa saba, mwaka wa kusamehe wadeni, uko karibu’; mkamfikiria ndugu yenu maskini kwa ukali na kukataa kumpa chochote; yeye aweza kumlilia Mwenyezi-Mungu dhidi yenu na hiyo ikawa dhambi kwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Angalieni wazo ovu lisiwaingie mioyoni mwenu, mkasema: ‘Mwaka wa saba, mwaka wa kusamehe wadeni, uko karibu’; mkamfikiria ndugu yenu maskini kwa ukali na kukataa kumpa chochote; yeye aweza kumlilia Mwenyezi-Mungu dhidi yenu na hiyo ikawa dhambi kwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Angalieni wazo ovu lisiwaingie mioyoni mwenu, mkasema: ‘Mwaka wa saba, mwaka wa kusamehe wadeni, uko karibu’; mkamfikiria ndugu yenu maskini kwa ukali na kukataa kumpa chochote; yeye aweza kumlilia Mwenyezi-Mungu dhidi yenu na hiyo ikawa dhambi kwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Jihadhari usijiwekee wazo hili ovu: “Mwaka wa saba, mwaka wa kufuta madeni umekaribia,” usije ukaonesha nia mbaya kwa ndugu yako mhitaji na ukaacha kumpa chochote. Anaweza kumlalamikia Mwenyezi Mungu dhidi yako nawe utakuwa umepatikana na hatia ya dhambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Jihadhari usijiwekee wazo hili ovu: “Mwaka wa saba, mwaka wa kufuta madeni umekaribia,” usije ukaonyesha nia mbaya kwa ndugu yako mhitaji na ukaacha kumpa chochote. Anaweza kumlalamikia bwana dhidi yako nawe utakuwa umepatikana na hatia ya dhambi.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 15:9
30 Marejeleo ya Msalaba  

Hata wakafanya kilio cha maskini kumfikia, Naye akasikia kilio cha hao wateswao.


Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.


Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.


Maana mlipiza kisasi cha damu awakumbuka, Hakukisahau kilio cha wanyonge.


Usimtese mjane yeyote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.


Ukiwatesa watu hao katika neno lolote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,


BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;


Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri.


Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa.


Usile mkate wa mtu mwenye husuda; Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa;


Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu.


Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri; Wala haufikiri uhitaji utakaomjia.


Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.


Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.


Mwisho wa kila mwaka wa saba kila mtu na amwache huru ndugu yake aliye Mwebrania, aliyeuzwa kwako na kukutumikia miaka sita utamwacha atoke kwako huru, lakini baba zenu hawakunisikiliza, wala hawakutega masikio yao.


Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;


Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?


Kila miaka saba, mwisho wake, fanya maachilio.


mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako.


Musa, akawaamuru, akasema, Mwisho wa kila mwaka wa saba, wakati wa maachilio, wakati ulioamriwa wa sikukuu ya vibanda,


Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.


Au mwadhani ya kwamba Maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?


Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliokosa kuwalipa kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.


Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.


Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung'unika;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo