Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 15:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 umwangalie kwa wema katika kundi lako, na sakafu yako ya nafaka, na kinu chako cha divai; mpe kama alivyokubarikia BWANA, Mungu wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Mpe kwa ukarimu kile ambacho Mwenyezi-Mungu amekubariki: Kondoo, nafaka na divai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Mpe kwa ukarimu kile ambacho Mwenyezi-Mungu amekubariki: Kondoo, nafaka na divai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Mpe kwa ukarimu kile ambacho Mwenyezi-Mungu amekubariki: kondoo, nafaka na divai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Mpe kwa hiari kutoka kundi lako la kondoo na mbuzi, kutoka sakafu yako ya kupuria nafaka, na kutoka shinikizo lako la kukamulia zabibu. Mpe kama vile Mwenyezi Mungu, Mungu wako, alivyokubariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Mpe kwa uhuru kutoka zizi lako la kondoo na mbuzi, kutoka sakafu yako ya kupuria nafaka na kutoka mashinikizo yako ya kukamulia divai. Mpe kama vile ambavyo bwana Mwenyezi Mungu wako alivyokubariki.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 15:14
8 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha akawaambia, Nendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyekuwa na kitu; maana siku hii ni takatifu kwa BWANA wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.


Ametoa kwa ukarimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.


Watu wako wakafanya makao ya huko; Ee Mungu, kwa wema wako uliwaruzuku walioonewa.


Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo.


Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.


Siku ya kwanza ya juma kila mmoja wenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;


Nawe utakapomwacha huru aondoke kwako, usimwache aende zake mikono mitupu;


Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, akakukomboa BWANA, Mungu wako; kwa hiyo mimi nakuamuru neno hili hivi leo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo