Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 15:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Maana maskini hawatakosekana nchini; hivyo nawaamuru, muwe wakarimu kwa ndugu zenu wahitaji na maskini nchini mwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Maana maskini hawatakosekana nchini; hivyo nawaamuru, muwe wakarimu kwa ndugu zenu wahitaji na maskini nchini mwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Maana maskini hawatakosekana nchini; hivyo nawaamuru, muwe wakarimu kwa ndugu zenu wahitaji na maskini nchini mwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Siku zote watakuwa watu maskini katika nchi. Kwa hiyo ninawaamuru mwe wakarimu kwa ndugu zenu walio maskini na wahitaji katika nchi yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Siku zote watakuwepo watu maskini katika nchi. Kwa hiyo ninawaamuru mwe na mikono iliyokunjuliwa kuwaelekea ndugu zenu, kuwaelekea maskini na wahitaji katika nchi yenu.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 15:11
17 Marejeleo ya Msalaba  

lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo hivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni.


Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.


Tajiri na maskini hukutana pamoja; BWANA ndiye aliyewaumba wote wawili.


Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.


wala hakumdhulumu mtu, bali amemrudishia mdeni wake rehani yake, wala hakumnyang'anya mtu mali yake kwa nguvu, naye amewapa wenye njaa chakula chake, na kuwavika nguo walio uchi;


Kwa maana siku zote mnao maskini pamoja nanyi; lakini mimi hamko nami siku zote.


Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.


maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamko nami sikuzote.


Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwizi, wala nondo haharibu.


Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamko nami sikuzote.


wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kulingana na haja ya kila mmoja.


Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini;


lakini mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo