Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 15:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia BWANA, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Mpeni ndugu maskini kwa ukarimu bila kunungunika; maana kwa ajili ya hayo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki katika kazi zenu zote na katika kila mfanyalo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Mpeni ndugu maskini kwa ukarimu bila kunungunika; maana kwa ajili ya hayo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki katika kazi zenu zote na katika kila mfanyalo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Mpeni ndugu maskini kwa ukarimu bila kunung'unika; maana kwa ajili ya hayo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki katika kazi zenu zote na katika kila mfanyalo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Mpe kwa ukarimu na ufanye hivyo bila kinyongo moyoni, ndipo kwa sababu ya hili Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atakubariki katika kazi zako zote na kwa kila kitu utakachokiwekea mkono wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Mpe kwa ukarimu na ufanye hivyo bila kinyongo moyoni, ndipo kwa sababu ya hili bwana Mwenyezi Mungu wenu atakubariki katika kazi zako zote na kwa kila kitu utakachokiwekea mkono wako.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 15:10
21 Marejeleo ya Msalaba  

Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa; Maana huwapa maskini chakula chake.


Tupa chakula chako juu ya maji; Maana utakiona baada ya siku nyingi.


Bali muungwana huwaza mambo ya kiungwana, naye hushika sana mambo ya kiungwana.


na kama ukimpa mtu mwenye njaa chakula chako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.


Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.


Katika mambo yote nimewaonesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.


mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; msimamizi, na asimamie kwa bidii; anayerehemu, na arehemu kwa furaha.


Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale.


na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.


Wala usione ugumu, utakapomwacha huru kuondoka kwako; kwani amekutumikia miaka sita kwa ujira mara mbili wa mwajiriwa; na BWANA, Mungu wako, atakubarikia kwa yote utakayofanya.


Lakini hawatakuwako maskini kwenu; (kwa kuwa BWANA atakubarikia kweli katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako;)


mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.


Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili BWANA, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako.


BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.


Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.


Mtu akisema, na aseme kama asemaye maneno halisi ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo