Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Kumbukumbu la Torati 14:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia BWANA, Mungu wako;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Ikiwa safari ni ndefu kwa kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amechagua mahali pa kuweka jina lake ambapo ni mbali mno na nyumbani, nanyi hamwezi kubeba zaka za mazao yenu ambayo Mwenyezi-Mungu amewajalia kupata, basi, fanyeni hivi:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Ikiwa safari ni ndefu kwa kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amechagua mahali pa kuweka jina lake ambapo ni mbali mno na nyumbani, nanyi hamwezi kubeba zaka za mazao yenu ambayo Mwenyezi-Mungu amewajalia kupata, basi, fanyeni hivi:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Ikiwa safari ni ndefu kwa kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amechagua mahali pa kuweka jina lake ambapo ni mbali mno na nyumbani, nanyi hamwezi kubeba zaka za mazao yenu ambayo Mwenyezi-Mungu amewajalia kupata, basi, fanyeni hivi:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Lakini ikiwa mahali pale ni mbali sana nanyi mmebarikiwa na Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na hamwezi kubeba zaka yenu (kwa sababu mahali pale Mwenyezi Mungu atakapopachagua kuliweka Jina lake ni mbali sana),

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Lakini ikiwa mahali pale ni mbali sana nanyi mmebarikiwa na bwana Mwenyezi Mungu wenu na hamwezi kubeba zaka yenu (kwa sababu mahali pale bwana atakapopachagua kuliweka Jina lake ni mbali sana),

Tazama sura Nakili

Kumbukumbu la Torati 14:24
5 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hadi bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako.

Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu.

Na mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apaweke jina lake, pakiwa mbali nawe mno, ndipo utakapochinja katika kundi lako la ng'ombe na kondoo alilokupa BWANA kama nilivyokuagiza, nawe utakula ndani ya malango yako, kwa kufuata yote inayotamani roho yako.

Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika makabila yenu yote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe uende huko;

ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo