Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 12:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 nawe zisongeze sadaka zako za kuteketezwa, nyama na damu, juu ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako; na damu ya dhabihu zako uimwage juu ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako, na wewe utakula nyama yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Hapo, mtatoa sadaka za kuteketezwa, nyama na damu, kwenye madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; damu ya mnyama mtainyunyiza kwenye madhabahu yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, lakini mnaruhusiwa kula nyama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Hapo, mtatoa sadaka za kuteketezwa, nyama na damu, kwenye madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; damu ya mnyama mtainyunyiza kwenye madhabahu yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, lakini mnaruhusiwa kula nyama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Hapo, mtatoa sadaka za kuteketezwa, nyama na damu, kwenye madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; damu ya mnyama mtainyunyiza kwenye madhabahu yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, lakini mnaruhusiwa kula nyama.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Leteni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, vyote nyama na damu. Damu ya dhabihu zenu lazima imiminwe kando ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, lakini nyama mnaweza kula.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Leteni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya madhabahu ya bwana Mwenyezi Mungu wenu, vyote nyama na damu. Damu ya dhabihu zenu lazima imiminwe kando ya madhabahu ya bwana Mwenyezi Mungu wenu, lakini nyama mnaweza kula.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 12:27
7 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tieni sadaka zenu za kuteketezwa pamoja na dhabihu zenu, mkale nyama.


lakini matumbo yake, na miguu yake, ataosha kwa maji; na huyo kuhani atavisongeza vyote na kuviteketeza juu ya madhabahu; ni sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA.


Naye atamchinja huyo ng'ombe mbele ya BWANA; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kandokando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania


lakini matumbo yake, na miguu yake, ataiosha kwa maji; na huyo kuhani ataviteketeza vyote juu ya madhabahu, ili iwe sadaka ya kuteketezwa, dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA.


Kwa kuwa uhai wa mwili uko katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.


Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng'ombe, dume au jike, atamtoa huyo asiye na dosari mbele ya BWANA.


Kisha kuhani atatwaa baadhi ya hiyo damu yake kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya kuteketeza na damu yake yote ataimwaga chini ya madhabahu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo