Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 12:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Hizi ndizo amri na hukumu mtakazofuataa kuzifanya katika nchi aliyokupa BWANA, Mungu wa baba zako, uimiliki, siku zote mtakazoishi juu ya nchi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 “Yafuatayo ni masharti na maagizo ambayo mtayatimiza katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, amewapa muimiliki, siku zote za maisha yenu nchini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 “Yafuatayo ni masharti na maagizo ambayo mtayatimiza katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, amewapa muimiliki, siku zote za maisha yenu nchini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 “Yafuatayo ni masharti na maagizo ambayo mtayatimiza katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, amewapa muimiliki, siku zote za maisha yenu nchini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Hizi ndizo amri na sheria ambazo ni lazima mwe waangalifu kuzifuata katika nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, amewapa kumiliki, kwa muda wote mtakaoishi katika nchi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Hizi ndizo amri na sheria ambazo ni lazima mwe waangalifu kuzifuata katika nchi ambayo bwana, Mungu wa baba zenu, amewapa kumiliki, kwa muda wote mtakaoishi katika nchi.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 12:1
16 Marejeleo ya Msalaba  

ili wakuche wewe siku zote watakazoishi katika nchi uliyowapa baba zetu.


Je! Mtu hana huduma ngumu juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa?


Nitamwimbia BWANA maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai;


Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako.


Nitamsifu BWANA muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.


Mimi ni BWANA, Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda;


Nanyi angalieni mzifanye amri na hukumu zote niwawekeazo leo mbele yenu.


Jilinde nafsi yako usimpuuze Mlawi siku zote utakazoishi katika nchi yako.


Nikawaamuru wakati huo, nikawaambia, BWANA, Mungu wenu, amewapa ninyi nchi hii muimiliki, basi vukeni ng'ambo wenye silaha mbele ya ndugu zenu, wana wa Israeli, nyote mlio mashujaa.


tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo BWANA, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.


haya ndiyo maagizo, amri na hukumu, Musa alizowaambia wana wa Israeli walipotoka Misri;


Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama BWANA, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki.


Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu nisemazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuzizingatia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo