Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 10:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Baba zako walienda Misri wakiwa watu sabini; na sasa BWANA, Mungu wako, amekufanya kama nyota za mbinguni kwa wingi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Babu zenu walipokwenda Misri, walikuwa watu sabini tu, lakini sasa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi kama nyota za mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Babu zenu walipokwenda Misri, walikuwa watu sabini tu, lakini sasa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi kama nyota za mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Babu zenu walipokwenda Misri, walikuwa watu sabini tu, lakini sasa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi kama nyota za mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Baba zako walioshuka kwenda Misri jumla yao walikuwa sabini, na sasa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, amekufanya taifa la watu wengi kama nyota za angani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Baba zako walioshuka kwenda Misri jumla yao walikuwa sabini, na sasa bwana Mwenyezi Mungu wako amekufanya wengi kama nyota za angani.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 10:22
14 Marejeleo ya Msalaba  

Akamtoa nje, akasema, Tazama juu mbinguni kisha uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.


katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;


Watu wote waliokuja pamoja na Yakobo mpaka Misri, waliokuwa wazawa wake, bila wake za wanawe, walikuwa watu sitini na sita.


Na wana wa Yusufu aliozaliwa katika Misri walikuwa wawili. Watu wote wa nyumba ya Yakobo walioingia Misri walikuwa sabini.


Watoto wao nao uliwaongeza kama nyota za mbinguni, ukawaingiza katika nchi ile, uliyowaambia baba zao kuwa wataingia kuimiliki.


Na wale watu wote waliotokana na uzao wa Yakobo walikuwa watu sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo.


Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, elfu mia sita na moja, mia saba na thelathini (601,730).


Na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu ishirini na tatu, kila mwanamume tangu huyo aliyepata umri wa mwezi mmoja, na zaidi; kwa kuwa hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli, kwa sababu hawakupewa urithi katika wana wa Israeli.


Yusufu akatuma watu akamwita Yakobo babaye na jamaa zake wote pia, watu sabini na watano.


BWANA, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi, nanyi, angalieni, mmekuwa leo mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi.


BWANA, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabariki, kama alivyowaahidi.


Nawe ujibu, ukaseme mbele za BWANA, Mungu wako, Baba yangu alikuwa Mwarami karibu na kupotea, akashuka Misri, akakaa huko ugenini, nao ni wachache hesabu yao; akawa taifa kubwa huko, yenye nguvu na watu wengi.


Nanyi mtasalia wachache kwa hesabu, ninyi mliokuwa mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi; kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako.


Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo