Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 10:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Tazama, mbingu ni mali ya BWANA, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Tazama, mbingu hata mbingu za mbingu ni mali yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; dunia na vyote vilivyomo ni mali yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Tazama, mbingu hata mbingu za mbingu ni mali yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; dunia na vyote vilivyomo ni mali yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Tazama, mbingu hata mbingu za mbingu ni mali yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; dunia na vyote vilivyomo ni mali yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo, ni mali ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, ni mali ya bwana Mwenyezi Mungu wako.

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 10:14
21 Marejeleo ya Msalaba  

Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.


Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu sana, Muumba mbingu na nchi,


Lakini Mungu je? Hakika atakaa juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga!


Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; seuze nyumba hii niliyoijenga!


Ezra akasema, Wewe ndiwe BWANA, wewe peke yako; wewe ulifanya mbingu, mbingu za mbingu, pamoja na jeshi lake lote, dunia na vyote vilivyomo, bahari na vitu vyote vilivyomo, nawe unavihifadhi vitu hivi vyote; na jeshi la mbinguni lakusujudu wewe.


Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe? Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.


Mbingu ni mbingu za BWANA, Bali nchi amewapa wanadamu.


Msifuni, enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu.


Nchi na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.


Kama ningekuwa na njaa singekuambia, Maana ulimwengu ni wangu, na vyote vilivyomo.


Apandaye mbingu za mbingu za tangu milele; Aitoa sauti yake, sauti ya nguvu.


Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,


Musa akamwambia, Mara nitakapotoka mjini nitamwinulia BWANA mikono yangu; na hizo ngurumo zitakoma, wala haitanyesha mvua ya mawe tena; ili upate kujua ya kuwa dunia hii ni ya BWANA.


BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?


Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;


maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.


Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyewaambia, na kwa ajili ya dhamiri.


Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.


kuzifuata amri za BWANA na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri?


Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo