Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 1:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Nchi hii yote nimeiweka mbele yenu. Basi, nendeni mkaimiliki nchi hiyo ambayo mimi Mwenyezi-Mungu niliapa kuwapa wazee wenu Abrahamu, Isaka, Yakobo na wazawa wao.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Nchi hii yote nimeiweka mbele yenu. Basi, nendeni mkaimiliki nchi hiyo ambayo mimi Mwenyezi-Mungu niliapa kuwapa wazee wenu Abrahamu, Isaka, Yakobo na wazawa wao.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Nchi hii yote nimeiweka mbele yenu. Basi, nendeni mkaimiliki nchi hiyo ambayo mimi Mwenyezi-Mungu niliapa kuwapa wazee wenu Abrahamu, Isaka, Yakobo na wazawa wao.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Tazama, nimewapa ninyi nchi hii. Ingieni mkaimiliki nchi ambayo Mwenyezi Mungu aliapa kuwa angewapa baba zenu, Ibrahimu, Isaka na Yakobo, pamoja na uzao wao baada yao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Tazama, nimewapa ninyi nchi hii. Ingieni mkaimiliki nchi ambayo bwana aliapa kuwa angaliwapa baba zenu, Ibrahimu, Isaka na Yakobo, pamoja na vizazi vyao baada yao.”

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 1:8
39 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.


Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana uovu wa Waamori haujatimia bado.


Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,


Ukawapa chakula toka mbinguni, kwa ajili ya njaa yao, na kwa ajili yao ukaleta maji kutoka mwambani, kwa sababu ya kiu yao, ukawaamuru waingie na kuimiliki, nchi ambayo umeinua mkono wako kuwapa.


Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hadi bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako.


BWANA akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii;


ukawapa nchi hii, uliyowaapia baba zao kwamba utawapa, nchi itiririkayo maziwa na asali;


Nanyi mtaimiliki, mtu huyu sawasawa na huyu; ambayo niliuinua mkono wangu kuwapa baba zenu; na nchi hii itawaangukia kuwa urithi.


hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona;


Hakika yangu hapana mtu mmoja katika wale watu waliotoka Misri, tangu huyo aliyepata umri wa miaka ishirini, na zaidi, atakayeiona hiyo nchi niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; kwa sababu hawakuniandama kwa moyo wote;


BWANA, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabariki, kama alivyowaahidi.


Hakika yangu hapana mmoja miongoni mwa watu hawa wa kizazi hiki kibaya atakayeiona nchi hiyo nzuri, niliyowaapia baba zenu kuwapa,


BWANA akaniambia, Ondoka, uendelee na safari yako ukiwaongoza watu; nao wataingia waimiliki nchi, niliyowaapia baba zao ya kuwa nitawapa.


Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu; tokea hilo jangwa, na Lebanoni, na tokea mto wa Frati, mpaka bahari ya magharibi, itakuwa ndiyo mipaka yenu.


nanyi mpate kuzifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, ya kuwa atawapa wao na kizazi chao, nchi imiminikayo maziwa na asali


kama walivyonifanyia hao wana wa Esau waishio Seiri, na hao Wamoabi waishio Ari; hata nivuke Yordani niingie nchi tupewayo na BWANA, Mungu wetu.


Uangalie kutoka makazi yako matakatifu mbinguni, uwabarikie watu wako Israeli, na nchi uliyotupa kama ulivyowaapia baba zetu, nchi imiminikayo maziwa na asali.


Ukamwendee kuhani atakayekuwapo siku zile, ukamwambie, Ninakiri leo kwa BWANA, Mungu wako, ya kuwa nimeingia katika nchi BWANA aliyowaapia baba zetu ya kwamba atatupa.


BWANA atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.


ili uingie katika agano la BWANA, Mungu wako, na kiapo chake, afanyacho nawe BWANA, Mungu wako, hivi leo;


kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.


Musa akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote, Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi BWANA aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha.


BWANA akamwambia, Hii ndiyo nchi niliyowaapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, nikisema, Nitawapa wazao wako. Basi nimekuonesha kwa macho yako, lakini hutavuka huko.


Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu.


Kisha BWANA Mungu wako atakapokuleta katika nchi aliyowaapia babu zako, Abrahamu na Isaka na Yakobo, ya kuwa atakupa; miji mikubwa mizuri usiyoijenga wewe,


Na itakuwa, kwa sababu mnazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi BWANA, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako;


naye atakupenda na kukubariki na kukuongeza tena ataubariki uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, kuongezeka kwa ng'ombe na kondoo wako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa.


bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kukitimiza kiapo chake alichowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.


Amri hii ninayokuamuru leo mtaizingatia, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo BWANA aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki.


Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya BWANA, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno BWANA alilowaapia baba zako Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.


Kwa maana Mungu, alipompa Abrahamu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake,


akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza.


Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.


Kisha malaika wa BWANA alikwea kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hadi nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo