Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kumbukumbu la Torati 1:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 BWANA, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabariki, kama alivyowaahidi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, na awafanye mzidi kuongezeka mara elfu zaidi ya mlivyo sasa na kuwabariki kama alivyoahidi!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, na awafanye mzidi kuongezeka mara elfu zaidi ya mlivyo sasa na kuwabariki kama alivyoahidi!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zenu, na awafanye mzidi kuongezeka mara elfu zaidi ya mlivyo sasa na kuwabariki kama alivyoahidi!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Naye Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zenu, na awaongeze mara elfu na kuwabariki kama alivyoahidi!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Naye bwana, Mungu wa baba zenu na awaongeze mara elfu na kuwabariki kama alivyoahidi!

Tazama sura Nakili




Kumbukumbu la Torati 1:11
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akamtoa nje, akasema, Tazama juu mbinguni kisha uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.


katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;


Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.


Naam, kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia; Kwa baraka za juu mbinguni. Baraka za vilindi vilivyo chini, Baraka za maziwa, na za mimba.


Naye Yoabu akamwambia mfalme, BWANA, Mungu wako, na awaongeze watu, hesabu yao ikiwa yoyote, mara mia, tena macho ya bwana wangu mfalme na yawaone; ila kwa nini neno hili limempendeza bwana wangu mfalme?


Naye Yoabu akasema, BWANA na awaongeze watu wake mara mia hesabu yao ilivyo; lakini, bwana wangu mfalme, si wote watumishi wa bwana wangu? Mbona basi bwana wangu analitaka neno hili? Mbona alete hatia kwa Israeli?


BWANA na awaongeze ninyi, Ninyi na watoto wenu.


Mkumbuke Abrahamu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.


Nilikufanya kuwa maelfu, kama mimea ya mashamba, ukaongezeka, na kuzidi kuwa mkubwa, ukapata kuwa na uzuri mno; matiti yako yakaumbwa, nywele zako zikawa zimeota; lakini ulikuwa uchi, bila mavazi.


Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa.


Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabariki.


BWANA, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi, nanyi, angalieni, mmekuwa leo mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi.


Nitachukuaje peke yangu mimi mwenyewe udhia wenu, na mzigo wenu, na ugomvi wenu?


Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.


Baba zako walienda Misri wakiwa watu sabini; na sasa BWANA, Mungu wako, amekufanya kama nyota za mbinguni kwa wingi.


Nanyi mtasalia wachache kwa hesabu, ninyi mliokuwa mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi; kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo