Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 66:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Katika kila sikukuu ya mwezi mpya, na katika kila siku ya Sabato, binadamu wote watakuja kuniabudu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Katika kila sikukuu ya mwezi mpya, na katika kila siku ya Sabato, binadamu wote watakuja kuniabudu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Katika kila sikukuu ya mwezi mpya, na katika kila siku ya Sabato, binadamu wote watakuja kuniabudu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Kutoka Mwezi Mpya hata mwingine, na kutoka Sabato hadi nyingine, wanadamu wote watakuja na kusujudu mbele zangu,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Kutoka Mwezi Mpya hata mwingine, na kutoka Sabato hadi nyingine, wanadamu wote watakuja na kusujudu mbele zangu,” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Isaya 66:23
25 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Kwa nini kumwendea leo? Sio mwandamo wa mwezi, wala sabato. Akasema, Si neno.


Maana ufalme ni wa BWANA, Naye ndiye awatawalaye mataifa.


Wewe usikiaye maombi, Wote wenye mwili watakujia.


Tutakapozidiwa na matendo maovu Wewe utatuondolea uovu wetu.


Mataifa yote uliyoyaumba watakuja; Watakusujudia Wewe, Bwana, Watalitukuza jina lako;


Na BWANA atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua BWANA katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea BWANA nadhiri, na kuzitekeleza.


Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hadi Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri.


Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.


Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu BWANA katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.


BWANA, mkombozi wa Israeli, Mtakatifu wake, amwambia hivi yeye anayedharauliwa na wanadamu; yeye anayechukiwa na taifa hili; yeye aliye mtumishi wao watawalao; Wafalme wataona, watasimama; wakuu nao watasujudu; kwa sababu ya BWANA aliye mwaminifu, Mtakatifu wa Israeli aliyekuchagua.


Kwa maana katika mlima wangu mtakatifu, katika mlima mrefu sana wa Israeli, asema Bwana MUNGU, ndiko watakakonitumikia nyumba yote ya Israeli, wote pia katika nchi ile; nami nitawatakabali huko, na huko nitataka matoleo yenu, na malimbuko ya dhabihu zenu, pamoja na vitu vyenu vitakatifu vyote.


Tena itakuwa kazi ya mkuu kutoa hizo sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na sadaka za vinywaji, katika sikukuu, na katika mwezi mpya, na katika sabato, katika sikukuu zote za nyumba ya Israeli zilizoamriwa; atatengeneza sadaka ya dhambi, na sadaka ya unga, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ya Israeli.


Bwana MUNGU asema hivi; Lango la ua wa ndani, lielekealo upande wa mashariki litafungwa siku sita za kazi; lakini siku ya sabato litafunguliwa, na siku ya mwezi mwandamo litafunguliwa.


Na siku ya mwezi mwandamo itakuwa ni ng'ombe dume mchanga mkamilifu; na wana-kondoo sita, na kondoo dume; nao watakuwa wakamilifu.


Yuda naye atafanya vita juu ya Yerusalemu; na huo utajiri wa mataifa wa pande zote utakusanywa, dhahabu, na fedha, na mavazi; vitu vingi sana.


Hata itakuwa, ya kwamba kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja kupigana na Yerusalemu, atakwea mwaka baada ya mwaka ili kumwabudu Mfalme, BWANA wa majeshi, na kuiadhimisha sikukuu ya Vibanda.


Na kama jamaa ya Misri hawakwei, wala hawaji, pia haitanyesha kwao; itakuwako tauni, ambayo BWANA atawapiga mataifa, wasiokwea ili kuadhimisha sikukuu ya Vibanda.


Hii ndiyo adhabu ya Misri, na adhabu ya mataifa yote, wasiokwea ili kuadhimisha sikukuu ya Vibanda.


Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.


Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.


Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo