Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Isaya 65:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na BWANA, na watoto wao pamoja nao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Kazi zao hazitakuwa bure, wala hawatazaa watoto wa kupata maafa; maana watakuwa waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu, wamebarikiwa wao pamoja na wazawa wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Kazi zao hazitakuwa bure, wala hawatazaa watoto wa kupata maafa; maana watakuwa waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu, wamebarikiwa wao pamoja na wazawa wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Kazi zao hazitakuwa bure, wala hawatazaa watoto wa kupata maafa; maana watakuwa waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu, wamebarikiwa wao pamoja na wazawa wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga, kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na Mwenyezi Mungu, wao na wazao wao pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga, kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na bwana, wao na wazao wao pamoja nao.

Tazama sura Nakili




Isaya 65:23
28 Marejeleo ya Msalaba  

nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;


Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.


Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao.


Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;


Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina BWANA, na thawabu yangu ina Mungu wangu.


Kwa nini mtoe fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.


Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika makabila ya watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na BWANA.


Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.


Nami nitawaokoeni kutoka kwa uchafu wenu wote; nitaiamuru ngano iongezeke, wala sitawaletea njaa tena.


na nguvu zenu mtazitumia bure; kwa kuwa nchi yenu haitazaa mazao yake, wala miti ya nchi haitazaa matunda yake.


Nami nitaleta wanyama wakali kati yenu, ambao watawanyang'anya watoto wenu, na kuwaharibu wanyama wenu wa kufugwa, na kuwapunguza hesabu yenu; na njia zenu zitakuwa ni ukiwa.


Nanyi mtakula nyama ya miili ya watoto wenu wa kiume, na nyama ya miili ya binti zenu mtaila.


Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamtosheki na vinywaji; mnajivika nguo lakini hampati joto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotobokatoboka.


Je, Mbegu ingali ghalani? Naam, huo mzabibu, wala mtini, wala mkomamanga, wala mzeituni, haikuzaa kitu; tangu siku hii ya leo nitawabariki.


Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.


Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.


Kwa hiyo ilitoka katika imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazawa wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Abrahamu; aliye baba yetu sisi sote;


Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.


Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Abrahamu, na warithi kulingana na ahadi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo