Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Isaya 65:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, watumishi wangu watakula, bali ninyi mtaona njaa; tazama, watumishi wangu watakunywa, bali ninyi mtaona kiu; tazama, watumishi wangu watafurahi, bali ninyi mtatahayarika;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nasema, watumishi wangu watakula, lakini nyinyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa, lakini nyinyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini nyinyi mtafedheheka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nasema, watumishi wangu watakula, lakini nyinyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa, lakini nyinyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini nyinyi mtafedheheka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nasema, watumishi wangu watakula, lakini nyinyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa, lakini nyinyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini nyinyi mtafedheheka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “Watumishi wangu watakula, lakini ninyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa lakini ninyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini ninyi mtaona haya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kwa hiyo hili ndilo asemalo bwana Mwenyezi: “Watumishi wangu watakula, lakini ninyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa lakini ninyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini ninyi mtaona haya.

Tazama sura Nakili




Isaya 65:13
23 Marejeleo ya Msalaba  

Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema.


Mwenye haki hula akaishibisha nafsi yake; Bali tumbo la mtu mbaya litaona njaa.


Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;


Maskini na wahitaji wanatafuta maji, wala hapana; ndimi zao zimekauka kwa kiu; mimi, BWANA, nitawasikia, mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.


Nitafunua vijito vya maji juu ya vilima, na chemchemi katikati ya mabonde; nitageuza jangwa kuwa ziwa la maji, na mahali pakavu kuwa vijito vya maji.


Watarudishwa nyuma, wataaibishwa sana, hao wanaotumainia sanamu za mawe, na kuziambia sanamu za madini, Ninyi ndinyi miungu yetu.


Tazama, wenziwe wote watatahayari; na mafundi, hao ni wanadamu; na wakusanyike pamoja, wakasimame; wataogopa na kutahayari pamoja.


Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike.


Hawataona njaa, wala hawataona kiu; joto halitawapiga, wala jua; kwa maana yeye aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza.


Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.


Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika muali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.


Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele.


Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.


Nanyi mtaona, na mioyo yenu itafurahi, na mifupa yenu itasitawi kama majani mabichi; na mkono wa BWANA utajulikana, uwaelekeao watumishi wake, naye atawaonea adui zake ghadhabu.


Lisikilizeni neno la BWANA, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe BWANA, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.


Nao watapita katikati yake, wamedhikika sana na kuwa na njaa; na itakuwa watakapoona njaa, watalalamika na kuapa kwa mfalme wao, na kwa Mungu wao, na kuelekeza nyuso zao juu;


Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na wapenzi wako watakwenda kufungwa; hakika wakati huo utatahayarika, na kufadhaika kwa sababu ya uovu wako wote.


Tena, wengi wa hao wanaolala katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.


Nao watakula, lakini hawatashiba; watafanya zinaa, lakini hawataongezeka; kwa sababu wameacha kumwangalia BWANA.


Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo