Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 63:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Nitasimulia fadhili za Mwenyezi-Mungu; nitataja matendo yake yote yastahiliyo sifa, kwa sababu ya yote aliyotutendea, wema wake mkuu aliowapa Waisraeli kwa huruma yake, kadiri ya wingi wa fadhili zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Nitasimulia fadhili za Mwenyezi-Mungu; nitataja matendo yake yote yastahiliyo sifa, kwa sababu ya yote aliyotutendea, wema wake mkuu aliowapa Waisraeli kwa huruma yake, kadiri ya wingi wa fadhili zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Nitasimulia fadhili za Mwenyezi-Mungu; nitataja matendo yake yote yastahiliyo sifa, kwa sababu ya yote aliyotutendea, wema wake mkuu aliowapa Waisraeli kwa huruma yake, kadiri ya wingi wa fadhili zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Nitasimulia kuhusu wema wa Mwenyezi Mungu, kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa, sawasawa na yote ambayo Mwenyezi Mungu ametenda kwa ajili yetu: naam, mambo mengi mema aliyoyatenda kwa ajili ya nyumba ya Israeli, sawasawa na huruma zake na wema wake mwingi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Nitasimulia juu ya wema wa bwana, kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa, sawasawa na yote ambayo bwana ametenda kwa ajili yetu: naam, mambo mengi mema aliyoyatenda kwa ajili ya nyumba ya Israeli, sawasawa na huruma zake na wema wake mwingi.

Tazama sura Nakili




Isaya 63:7
46 Marejeleo ya Msalaba  

Hata siku ya nane akaagana na watu, nao wakambarikia mfalme, wakaenda hemani kwao, wakifurahi na kuchangamka moyoni kwa wema wote BWANA aliomfanyia Daudi mtumishi wake, na Israeli watu wake.


Akawaruhusu watu waende hemani kwao siku ya ishirini na tatu, ya mwezi wa saba, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote BWANA aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli watu wake.


Wakaitwaa miji yenye ngome, na nchi yenye utajiri, wakazitamalaki nyumba zilizojaa vitu vyema, visima vilivyochimbwa, mizabibu, na mizeituni, na miti mingi yenye matunda; hivyo wakala, wakashiba, wakanenepa, wakajifurahisha katika wema wako mwingi.


Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.


Ila kwa rehema zako nyingi hukuwakomesha kabisa, wala kuwaacha; kwa maana wewe u Mungu mwenye neema na rehema.


Kwa kuwa hawakukutumikia wewe katika ufalme wao, na katika wema wako mkuu uliowapa, na katika nchi ile kubwa yenye neema uliyowapa mbele yao, wala hawakubadili nia na kuyaacha mabaya yao.


Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote.


Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.


Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.


Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.


Na wamshukuru BWANA, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.


Watasimulia juu ya ukuu wa wema wako mwingi. Na wataiimba haki yako kwa sauti.


Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani.


Ee Mungu, unirehemu, kulingana na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.


Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu.


Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.


Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.


Kuzitangaza rehema zako asubuhi, Na uaminifu wako wakati wa usiku.


Yethro alifurahi kwa ajili ya wema wote BWANA aliowatendea Israeli, kwa alivyowaokoa mikononi mwa Wamisri.


Ee BWANA, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.


Mwangalieni Abrahamu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nilimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.


Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye.


Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakurudisha.


Kwa ghadhabu ifurikayo nilikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema BWANA, Mkombozi wako.


Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.


Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?


Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.


Nami nitakuposa uwe wangu wa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.


Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi! Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi! Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake.


Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu zawadi njema, je! Si Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema zaidi wao wamwombao?


Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?


Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;


Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;


Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo