Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Isaya 63:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Ndipo walipokumbuka siku za zamani, wakati wa Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu. Wakauliza, “Yuko wapi sasa Mwenyezi-Mungu, aliyewaokoa wachungaji wa kundi lake baharini? Yuko wapi yule aliyeiweka roho yake takatifu kati yao,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Ndipo walipokumbuka siku za zamani, wakati wa Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu. Wakauliza, “Yuko wapi sasa Mwenyezi-Mungu, aliyewaokoa wachungaji wa kundi lake baharini? Yuko wapi yule aliyeiweka roho yake takatifu kati yao,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Ndipo walipokumbuka siku za zamani, wakati wa Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu. Wakauliza, “Yuko wapi sasa Mwenyezi-Mungu, aliyewaokoa wachungaji wa kundi lake baharini? Yuko wapi yule aliyeiweka roho yake takatifu kati yao,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ndipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita, siku za Musa na watu wake: yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari, pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yule aliyeweka Roho wake Mtakatifu katikati yao,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ndipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita, siku za Musa na watu wake: yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari, pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yule aliyeweka Roho wake Mtakatifu katikati yao,

Tazama sura Nakili




Isaya 63:11
34 Marejeleo ya Msalaba  

Ukawapa na roho yako mwema ili kuwaelimisha, wala hukuwanyima mana vinywani mwao, tena ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao.


Lakini aliyaangalia mateso yao, Aliposikia kilio chao.


Akawakumbukia agano lake; Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;


Akaikemea Bahari ya Shamu ikakauka, Akawaongoza vilindini kana kwamba ni nchi kavu.


Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako.


Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani.


Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.


Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako.


Uliwaongoza watu wako kama kundi, Kwa mkono wa Musa na Haruni.


Kisha akawaongoza watu wake kama kondoo, Akawachunga kama kundi jangwani.


Wana wa Israeli wakaenda ndani wakipita kwenye nchi kavu ndani ya bahari; huku maji yakiwa ukuta kwao mkono wa kulia na mkono wa kushoto.


Ndivyo BWANA alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni mwa bahari, wamekufa.


BWANA asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu;


Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.


Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.


Wala hawakusema, Yuko wapi BWANA, aliyetutoa katika nchi ya Misri; akatuongoza jangwani, katika nchi ya ukame na mashimo, katika nchi ya kiu na ya kivuli cha mauti, katika nchi ambayo ndani yake hapiti mtu, wala haikukaliwa na watu?


Bali hatimaye Danieli akaingia mbele yangu, ambaye jina lake ni Belteshaza, kwa kufuata jina la mungu wangu; tena ndani yake inakaa roho ya miungu watakatifu; nikamsimulia ile ndoto, nikisema,


Na kwa nabii BWANA alimtoa Israeli katika Misri, Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.


Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale;


kama ilivyo ahadi niliyowawekea mlipotoka katika nchi ya Misri; na roho yangu inakaa kati yenu; msiogope.


Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.


Nami nitashuka niseme nawe huko, nami nitatwaa sehemu ya roho iliyo juu yako na kuiweka juu yao; nao watachukua mzigo wa watu hawa pamoja nawe, ili usiuchukue wewe peke yako.


Ndipo BWANA akashuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa, akaitia juu ya wale wazee sabini; ikawa, roho hiyo ilipowashukia, wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena.


Musa akamwambia, Je! Umekuwa na wivu kwa ajili yangu; ingekuwa heri kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii na kama BWANA angewatia roho yake.


Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu,


Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo