Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Isaya 62:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefziba; na nchi yako Beula; kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Hutaitwa tena: “Aliyeachwa”, wala nchi yako haitaitwa: “Ukiwa”. Bali utaitwa: “Namfurahia,” na nchi yako itaitwa: “Aliyeolewa.” Maana Mwenyezi-Mungu amependezwa nawe, naye atakuwa kama mume wa nchi yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Hutaitwa tena: “Aliyeachwa”, wala nchi yako haitaitwa: “Ukiwa”. Bali utaitwa: “Namfurahia,” na nchi yako itaitwa: “Aliyeolewa.” Maana Mwenyezi-Mungu amependezwa nawe, naye atakuwa kama mume wa nchi yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Hutaitwa tena: “Aliyeachwa”, wala nchi yako haitaitwa: “Ukiwa”. Bali utaitwa: “Namfurahia,” na nchi yako itaitwa: “Aliyeolewa.” Maana Mwenyezi-Mungu amependezwa nawe, naye atakuwa kama mume wa nchi yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Hawatakuita tena Aliyeachwa, wala nchi yako kuiita Ukiwa. Bali utaitwa Hefsiba, nayo nchi yako itaitwa Beula, kwa maana Mwenyezi Mungu atakufurahia, nayo nchi yako itaolewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Hawatakuita tena Aliyeachwa, wala nchi yako kuiita Ukiwa. Bali utaitwa Hefsiba, nayo nchi yako itaitwa Beula, kwa maana bwana atakufurahia, nayo nchi yako itaolewa.

Tazama sura Nakili




Isaya 62:4
32 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.


Nao watakatifu waliopo duniani, ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.


Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau.


Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na uchungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.


Na kwa kuwa umeachwa na kuchukiwa, Hata ikawa hapana mtu aliyepita ndani yako, Nitakufanya kuwa fahari ya milele, Furaha ya vizazi vingi.


Jeuri haitasikiwa tena katika nchi yako, Ukiwa na uharibifu hazitakuwa mipakani mwako; Bali utaziita kuta zako, Wokovu, Na malango yako, Sifa.


Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.


Nao watawaita, Watu watakatifu, Waliokombolewa na BWANA; Nawe utaitwa, Aliyetafutwa, Mji usioachwa.


Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha BWANA.


Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.


Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikika ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.


Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hadi Sayuni;


Naam, nitafurahi juu yao niwatendee mema, nami nitawapanda katika nchi hii kweli kweli, kwa moyo wangu wote, na kwa roho yangu yote.


Na mji huu utakuwa kwangu jina la furaha, na sifa na utukufu, mbele ya mataifa yote ya dunia, watakaosikia habari ya mema yote niwatendeayo, nao wataogopa na kutetemeka, kwa sababu ya mema yote na amani nitakaoupatia mji huo.


Nao watasema, Nchi hii, iliyokuwa ukiwa, imekuwa kama bustani ya Adeni; nayo miji iliyokuwa mahame, na ukiwa, na magofu, sasa ina maboma, inakaliwa na watu.


Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika, asema BWANA; nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi;


nayo nchi itaiitikia nafaka na divai na mafuta; nayo yataiitikia Yezreeli.


BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.


Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.


Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi.


Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa niliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.


Na BWANA, Mungu wako, atakufanya uwe na wingi wa uheri katika kazi yote ya mkono wako, katika uzao wa tumbo lako, na katika uzao wa ng'ombe wako, na katika uzao wa nchi yako; kwa kuwa BWANA atafurahi tena juu yako kwa wema, kama alivyofurahi juu ya baba zako;


Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.


ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.


Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo