Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 60:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Jua lako halitashuka tena, Wala mwezi wako hautajitenga; Kwa kuwa BWANA mwenyewe atakuwa nuru yako ya milele; Na siku za kuomboleza kwako zitakoma.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Mwanga wako mchana hautatua kama jua, wala mwangaza wako usiku kufifia kama mbalamwezi; maana Mwenyezi-Mungu ni mwanga wako milele, nazo siku zako za kuomboleza zitakoma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Mwanga wako mchana hautatua kama jua, wala mwangaza wako usiku kufifia kama mbalamwezi; maana Mwenyezi-Mungu ni mwanga wako milele, nazo siku zako za kuomboleza zitakoma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Mwanga wako mchana hautatua kama jua, wala mwangaza wako usiku kufifia kama mbalamwezi; maana Mwenyezi-Mungu ni mwanga wako milele, nazo siku zako za kuomboleza zitakoma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Jua lako halitazama tena, nao mwezi wako hautafifia tena; Mwenyezi Mungu atakuwa nuru yako milele, nazo siku zako za huzuni zitakoma.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Jua lako halitazama tena, nao mwezi wako hautafifia tena; bwana atakuwa nuru yako milele, nazo siku zako za huzuni zitakoma.

Tazama sura Nakili




Isaya 60:20
19 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?


Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.


Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa BWANA wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.


Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.


Kwa maana watu watakaa katika Sayuni huko Yerusalemu; wewe hutalia tena; hakika yake atakuonea rehema nyingi kwa sauti ya kilio chako; asikiapo ndipo atakapokujibu.


Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile BWANA atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha lao.


Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitatoweka.


Nao waliokombolewa na BWANA watarejea, Watafika Sayuni, wakiimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; Watapata shangwe na furaha; Huzuni na kuugua zitakimbia.


Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia.


kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.


Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikika ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.


Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni, wataukimbilia wema wa BWANA, nafaka, na divai, na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng'ombe; na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji; wala hawatahuzunika tena kabisa.


Ee BWANA, utugeuze kwako, nasi tutageuka; Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale.


Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue wakati wa adhuhuri, nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana.


lakini itakuwa siku moja, iliyojulikana na BWANA; si mchana, wala si usiku; lakini itakuwa, ya kwamba wakati wa jioni kutakuwako nuru.


Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini.


Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo.


Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo