Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 60:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Jua halitakuwa nuru yako tena wakati wa mchana, Wala mwezi hautakupa nuru kwa mwangaza wake; Bali BWANA atakuwa nuru ya milele kwako, Na Mungu wako atakuwa utukufu wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 “Hutahitaji tena jua kukuangazia mchana, wala mwezi kukumulikia usiku; maana mimi Mwenyezi-Mungu ni mwanga wako milele; mimi Mungu wako nitakuwa fahari yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 “Hutahitaji tena jua kukuangazia mchana, wala mwezi kukumulikia usiku; maana mimi Mwenyezi-Mungu ni mwanga wako milele; mimi Mungu wako nitakuwa fahari yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 “Hutahitaji tena jua kukuangazia mchana, wala mwezi kukumulikia usiku; maana mimi Mwenyezi-Mungu ni mwanga wako milele; mimi Mungu wako nitakuwa fahari yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Jua halitakuwa tena nuru yako mchana, wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia, kwa maana Mwenyezi Mungu atakuwa nuru yako ya milele, naye Mungu wako atakuwa utukufu wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Jua halitakuwa tena nuru yako mchana, wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia, kwa maana bwana atakuwa nuru yako ya milele, naye Mungu wako atakuwa utukufu wako.

Tazama sura Nakili




Isaya 60:19
21 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.


Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima, Katika nuru yako tutaona nuru.


Enyi wanadamu, hadi lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo hadi lini?


Kwa Mungu wokovu wangu, Na utukufu wangu; Mwamba wa nguvu zangu, Na kimbilio langu ni kwa Mungu.


Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.


Ee BWANA wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.


Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya BWANA.


Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa BWANA wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.


Katika siku ile BWANA wa majeshi atakuwa ni taji la fahari, na kilemba cha uzuri, kwa mabaki ya watu wake.


Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile BWANA atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha lao.


Utawapepeta, na upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfurahia BWANA, utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli.


Katika BWANA wazao wote wa Israeli watapewa haki, na kutukuka.


Nao waliokombolewa na BWANA watarejea, Watafika Sayuni, wakiimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; Watapata shangwe na furaha; Huzuni na kuugua zitakimbia.


Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia.


Watu wale waliokwenda katika giza Wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza.


Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.


Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka ya hao waliowatumikia; nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma.


Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.


Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako.


Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo.


Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo