Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Isaya 59:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Na Mkombozi atakuja Sayuni, kwa wao wa Yakobo waachao maasi yao, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Naye atakuja Siyoni kama Mkombozi, Mkombozi wa wazawa wa Yakobo ambao wataachana na makosa yao. Asema Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Naye atakuja Siyoni kama Mkombozi, Mkombozi wa wazawa wa Yakobo ambao wataachana na makosa yao. Asema Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Naye atakuja Siyoni kama Mkombozi, Mkombozi wa wazawa wa Yakobo ambao wataachana na makosa yao. Asema Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 “Mkombozi atakuja Sayuni, kwa wale wa Yakobo wanaozitubu dhambi zao,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 “Mkombozi atakuja Sayuni, kwa wale wa Yakobo wanaozitubu dhambi zao,” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Isaya 59:20
18 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.


Mabaki, nao ni mabaki ya Yakobo, watamrudia Mungu, aliye mwenye nguvu.


Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki.


Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema, Panda juu ya mlima mrefu; Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema, Paza sauti kwa nguvu; Paza sauti yako, usiogope; Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu.


Utanyonya maziwa ya mataifa, Utanyonya matiti ya wafalme; Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, Na mkombozi wako, Mwenye enzi wa Yakobo.


Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake iko pamoja naye, Na malipo yake yako mbele zake.


Kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Musa, mabaya haya yote yametupata lakini hata hivyo hatukumwomba BWANA, Mungu wetu, atupe fadhili zake, ili tugeuke na kuyaacha maovu yetu, na kuitambua kweli yake.


Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA.


bali kwanza niliwahubiria wale wa Dameski na Yerusalemu, na katika nchi yote ya Yudea, na watu wa Mataifa, kwamba watubu na kumwelekea Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.


Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;


Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabariki kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.


Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo