Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 59:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Toka magharibi hadi mashariki, kila mtu atamcha Mwenyezi-Mungu na kutambua utukufu wake. Maana atakuja kama mto uendao kasi, mto unaosukumwa kwa upepo wa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Toka magharibi hadi mashariki, kila mtu atamcha Mwenyezi-Mungu na kutambua utukufu wake. Maana atakuja kama mto uendao kasi, mto unaosukumwa kwa upepo wa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Toka magharibi hadi mashariki, kila mtu atamcha Mwenyezi-Mungu na kutambua utukufu wake. Maana atakuja kama mto uendao kasi, mto unaosukumwa kwa upepo wa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Kuanzia magharibi, watu wataliogopa jina la Mwenyezi Mungu na kuanzia mawio ya jua, watauheshimu utukufu wake. Adui atakapokuja kama mafuriko, Roho wa Mwenyezi Mungu atainua kiwango dhidi yake na kumshinda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Kuanzia magharibi, watu wataliogopa jina la bwana na kuanzia mawio ya jua, watauheshimu utukufu wake. Wakati adui atakapokuja kama mafuriko, Roho wa bwana atainua kiwango dhidi yake na kumshinda.

Tazama sura Nakili




Isaya 59:19
25 Marejeleo ya Msalaba  

Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la BWANA husifiwa.


Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.


Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu. Umewapa urithi wao waliogopao jina lako.


Tazama, jina la BWANA linakuja kutoka mbali sana, linawaka kwa hasira yake, kwa moshi mwingi sana unaopaa juu; midomo yake imejaa ghadhabu, na ulimi wake ni moto uangamizao;


na pumzi yake ni kijito kifurikacho, kifikacho hata shingoni, kupepeta mataifa kwa ungo wa ubatili; na lijamu ikoseshayo itakuwa katika taya za watu.


ili wapate kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.


Tazama, hawa watakuja kutoka mbali; na tazama, hawa kutoka kaskazini, na kutoka magharibi, na hawa kutoka nchi ya Sinimu.


Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa.


basi sasa angalia; Bwana aleta juu yao maji ya huo Mto, yenye nguvu, mengi sana, nayo ni mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; naye atakuja, na kupita juu ya mifereji yake yote, atafurika juu ya kingo zake zote;


Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye Juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.


Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.


Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.


Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.


Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;


Hapo ndipo atakapofunuliwa yule mwasi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa dhihirisho la kuja kwake;


Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.


Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo