Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Isaya 58:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 ndipo utakapojifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 utapata furaha yako kwangu mimi Mwenyezi-Mungu, nitakupatia ushindi katika kila pingamizi nchini, nitakulisha mali ya Yakobo, babu yako. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 utapata furaha yako kwangu mimi Mwenyezi-Mungu, nitakupatia ushindi katika kila pingamizi nchini, nitakulisha mali ya Yakobo, babu yako. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 utapata furaha yako kwangu mimi Mwenyezi-Mungu, nitakupatia ushindi katika kila pingamizi nchini, nitakulisha mali ya Yakobo, babu yako. Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 ndipo utakapojipatia furaha yako katika Mwenyezi Mungu, nami nitakufanya upande juu ya miinuko ya nchi na kusherehekea urithi wa Yakobo baba yako.” Kinywa cha Mwenyezi Mungu kimenena haya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 ndipo utakapojipatia furaha yako katika bwana, nami nitakufanya upande juu ya miinuko ya nchi na kusherehekea urithi wa Yakobo baba yako.” Kinywa cha bwana kimenena haya.

Tazama sura Nakili




Isaya 58:14
23 Marejeleo ya Msalaba  

Kwani ndipo utakapojifurahisha katika Mwenyezi, Na kuinua uso wako kumwelekea Mungu.


Je! Atajifurahisha katika Mwenyezi, Na kumlingana Mungu nyakati zote?


Kwa kuwa amenena, Haimfai mtu lolote Kujifurahisha na Mungu.


Akaitoa nchi yao iwe urithi, Urithi wa Israeli watu wake.


Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha kutoka mto wa furaha zako.


Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani.


Nawe ujifurahishe katika BWANA, Naye atakutimizia haja za moyo wako.


Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.


Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya.


Na utukufu wa BWANA utafunuliwa, Na watu wote watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.


Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.


Lakini mimi nilisema, Nitawezaje kukuweka pamoja na watoto, na kukupa nchi ipendezayo, urithi ulio mwema wa mataifa? Nami nikasema, Mtaniita, Baba yangu, wala hamtageuka na kuacha kunifuata.


Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu adui amesema juu yenu, Aha! Na, Mahali pa juu pa zamani pamekuwa petu tupamiliki;


Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha BWANA wa majeshi kimesema hivi.


Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.


Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;


U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.


Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.


Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo