Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 56:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Kwa maana BWANA awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Maana mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Towashi ashikaye sheria zangu za Sabato, anayefanya mambo yanayonipendeza, na kulizingatia agano langu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Maana mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Towashi ashikaye sheria zangu za Sabato, anayefanya mambo yanayonipendeza, na kulizingatia agano langu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Maana mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Towashi ashikaye sheria zangu za Sabato, anayefanya mambo yanayonipendeza, na kulizingatia agano langu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kwa matowashi washikao Sabato zangu, ambao huchagua kile kinachonipendeza na kulishika sana agano langu:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kwa kuwa hili ndilo asemalo bwana: “Kwa matowashi washikao Sabato zangu, ambao huchagua kile kinachonipendeza na kulishika sana agano langu:

Tazama sura Nakili




Isaya 56:4
12 Marejeleo ya Msalaba  

Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA? Kwa kuwa amefanya nami agano la milele; Ina taratibu katika yote, ni thabiti, Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote.


Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele, Maana ndizo changamko la moyo wangu.


Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.


Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami.


Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.


Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wowote.


Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;


Kama ukigeuza mguu wako usiivunje sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;


Watauliza njia ya kwenda Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njooni ninyi, mjiunge na BWANA, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa.


lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hatanyang'anywa.


Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati;


Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo