Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 56:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 BWANA asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu uko karibu kuja, na haki yangu kufunuliwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mwenyezi-Mungu asema: “Zingatieni haki na kutenda mema, maana nitawaokoeni hivi karibuni, watu wataona wazi kwamba ninawakomboeni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mwenyezi-Mungu asema: “Zingatieni haki na kutenda mema, maana nitawaokoeni hivi karibuni, watu wataona wazi kwamba ninawakomboeni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mwenyezi-Mungu asema: “Zingatieni haki na kutenda mema, maana nitawaokoeni hivi karibuni, watu wataona wazi kwamba ninawakomboeni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Dumisheni haki na mkatende lile lililo sawa, kwa maana wokovu wangu u karibu na haki yangu itafunuliwa upesi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Hili ndilo asemalo bwana: “Dumisheni haki na mkatende lile lililo sawa, kwa maana wokovu wangu u karibu na haki yangu itafunuliwa upesi.

Tazama sura Nakili




Isaya 56:1
26 Marejeleo ya Msalaba  

Heri washikao hukumu, Na kutenda haki sikuzote.


Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonesha wokovu wa Mungu.


Hakika wokovu wake uko karibu na wamchao, Ndipo utukufu wake ukae katika nchi yetu.


BWANA ametukuka; kwa maana anakaa juu; amejaza Sayuni hukumu na haki.


Mimi ninaleta karibu haki yangu, haitakuwa mbali, na wokovu wangu hautakawia; nami nitaweka wokovu katika Sayuni kwa ajili ya Israeli, utukufu wangu.


Haki yangu i karibu, wokovu wangu umekuwa wazi, na mikono yangu itawahukumu makabila ya watu; visiwa vitaningoja, navyo vitautumainia mkono wangu.


Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.


Maana mimi, BWANA, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wizi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele.


Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?


Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kumaliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia mhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.


Ni mfanya biashara, aliye na mizani ya udanganyifu mkononi mwake; anapenda kudhulumu.


Ee mwanadamu, yeye amekuonesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!


Nitaivumilia ghadhabu ya BWANA, kwa kuwa nimemwasi; hata atakaponitetea shutuma yangu, na kunifanyia hukumu; atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.


Ikumbukeni Torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.


Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.


Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.


Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hadi imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo