Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 54:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 “Nitafanya kama nilivyofanya wakati wa Noa: Wakati ule niliapa kwamba sitaifunika tena ardhi kwa gharika. Basi sasa naapa kwamba sitakukasirikia tena wala sitakukemea tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 “Nitafanya kama nilivyofanya wakati wa Noa: Wakati ule niliapa kwamba sitaifunika tena ardhi kwa gharika. Basi sasa naapa kwamba sitakukasirikia tena wala sitakukemea tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 “Nitafanya kama nilivyofanya wakati wa Noa: wakati ule niliapa kwamba sitaifunika tena ardhi kwa gharika. Basi sasa naapa kwamba sitakukasirikia tena wala sitakukemea tena.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Nuhu, nilipoapa kuwa maji ya Nuhu kamwe hayatafunika tena dunia. Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi, kamwe sitawakemea tena.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Nuhu, nilipoapa kuwa maji ya Nuhu kamwe hayatafunika tena dunia. Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi, kamwe sitawakemea tena.

Tazama sura Nakili




Isaya 54:9
18 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. 1


Kwa kuwa utasahau mateso yako; Utayakumbuka kama maji yaliyokwisha pita;


Umeweka mpaka yasiupite, Wala yasirudi kuifunikiza nchi.


Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.


Inua macho yako, ukatazame pande zote; hao wote wanajikusanya na kukujia. Kama niishivyo, asema BWANA, hakika utajivika hao wote kama pambo, nawe utajipamba kwao kama bibi arusi.


BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena;


Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na ukombozi wangu hautakoma kamwe.


Maana nondo atawala kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na wokovu wangu hata vizazi vyote.


ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.


BWANA ameapa kwa mkono wake wa kulia, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi.


BWANA asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyoyatenda, asema BWANA.


Hivyo ndivyo nitakavyoshibisha ghadhabu yangu juu yako, na wivu wangu utanitoka, nami nitatulia wala sitaona hasira tena.


Nanyi mtashibishwa mezani pangu kwa farasi, na magari ya vita, na mashujaa, na watu wote wa vita, asema Bwana MUNGU.


wala sitawaficha uso wangu tena; kwa maana nimemwaga roho yangu juu ya nyumba ya Israeli, asema Bwana MUNGU.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo