Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Isaya 54:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Maana BWANA amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 “Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewe kama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika, mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa. Mungu wako anasema:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 “Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewe kama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika, mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa. Mungu wako anasema:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 “Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewe kama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika, mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa. Mungu wako anasema:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Mwenyezi Mungu atakuita urudi kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni; kama mke aliyeolewa bado angali kijana na kukataliwa,” asema Mungu wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 bwana atakuita urudi kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni; kama mke aliyeolewa bado angali kijana na kukataliwa,” asema Mungu wako.

Tazama sura Nakili




Isaya 54:6
13 Marejeleo ya Msalaba  

Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako.


Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana hiyo ni sehemu yako ya maisha; na katika kazi zako unazozifanya chini ya jua.


Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefziba; na nchi yako Beula; kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa.


Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya majeraha yako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, mji ambao hakuna mtu autakaye.


Nami nitakuposa uwe wangu wa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.


Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu BWANA amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, ingawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.


Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.


Lakini Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo