Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 54:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na uchungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Imba kwa shangwe ewe uliye tasa, wewe ambaye hujapata kuzaa! Paza sauti na kuimba kwa nguvu, wewe usiyepata kujifungua mtoto. Maana watoto wako wewe uliyeachwa watakuwa wengi kuliko wa aliye na mume.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Imba kwa shangwe ewe uliye tasa, wewe ambaye hujapata kuzaa! Paza sauti na kuimba kwa nguvu, wewe usiyepata kujifungua mtoto. Maana watoto wako wewe uliyeachwa watakuwa wengi kuliko wa aliye na mume.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Imba kwa shangwe ewe uliye tasa, wewe ambaye hujapata kuzaa! paza sauti na kuimba kwa nguvu, wewe usiyepata kujifungua mtoto. Maana watoto wako wewe uliyeachwa watakuwa wengi kuliko wa aliye na mume.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 “Imba, ewe mwanamke tasa, wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto; paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha, wewe ambaye kamwe hukupata uchungu; kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 “Imba, ewe mwanamke tasa, wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto; paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha, wewe ambaye kamwe hukupata utungu; kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi kuliko wa mwanamke mwenye mume,” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Isaya 54:1
21 Marejeleo ya Msalaba  

Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami.


Humweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.


Kwetu sisi tuna dada mdogo, Wala hana matiti; Tumfanyieje dada yetu, Siku atakapoposwa?


Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.


Hawa watainua sauti zao, watapiga kelele; kwa sababu ya utukufu wa BWANA watapiga kelele toka baharini.


Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana BWANA amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli.


Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi; Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima; Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, Naye atawahurumia watu wake walioteswa.


Maana kuhusu mahali pako palipokuwa ukiwa, pasipokaliwa na watu, na nchi yako iliyoharibika hakika sasa utakuwa mwembamba usiwatoshe wenyeji wako, nao waliokumeza watakuwa mbali.


Watoto ulionyang'anywa watasema masikioni mwako, Mahali hapa ni pembamba, hapanitoshi; nipe nafasi nipate kukaa.


Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefziba; na nchi yako Beula; kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa.


Kabla hajawa na uchungu alizaa; Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto wa kiume.


Imba, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee Israeli; Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, Ee binti Yerusalemu.


Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.


Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na uchungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume.


Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Lakini waliokuwa na njaa sasa hawana njaa tena. Naam, huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini aliye na watoto wengi amehuzunika.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo