Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 52:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Basi sasa, nafanya nini hapa, asema BWANA, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema BWANA, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Katika hali ya sasa napata faida gani kuwaona watu wangu wamepelekwa utumwani? Hao wanaowatawala wanajitapa. Nalo jina langu laendelea kudharauliwa kila siku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Katika hali ya sasa napata faida gani kuwaona watu wangu wamepelekwa utumwani? Hao wanaowatawala wanajitapa. Nalo jina langu laendelea kudharauliwa kila siku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Katika hali ya sasa napata faida gani kuwaona watu wangu wamepelekwa utumwani? Hao wanaowatawala wanajitapa. Nalo jina langu laendelea kudharauliwa kila siku.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 “Basi sasa nina nini hapa?” asema Mwenyezi Mungu. “Kwa kuwa watu wangu wamechukuliwa pasipo malipo, nao wale wanaowatawala wanawadhihaki,” asema Mwenyezi Mungu. “Mchana kutwa jina langu limetukanwa bila kikomo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 “Basi sasa nina nini hapa?” asema bwana. “Kwa kuwa watu wangu wamechukuliwa pasipo malipo, nao wale wanaowatawala wanawadhihaki,” asema bwana. “Mchana kutwa jina langu limetukanwa bila kikomo.

Tazama sura Nakili




Isaya 52:5
27 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika atakufa.


Wawauza watu wako bila kupata mali, Wala hukupata faida kwa thamani yao.


Kwa sauti ya mwenye kulaumu na kukufuru, Kwa sababu ya adui na mjilipiza kisasi.


Ee Mungu, mtesi atalaumu hata lini? Adui alidharau jina lako hata milele?


Ee BWANA, uyakumbuke hayo, adui amelaumu, Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako.


BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;


Unafanyaje hapa? Nawe una nani hapa? Hata ukachimba kaburi hapa; ukamchimbia kaburi huko juu, na kumchongea makao katika jabali!


Lakini nakujua, kuketi kwako, na kutoka kwako, na kuingia kwako; na ghadhabu yako uliyonighadhibikia.


Isaya akawaambia, Mwambieni bwana wenu maneno haya; BWANA asema hivi, Usiyaogope maneno uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana.


Nilikuwa nimekasirika na watu wangu, niliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; kwa wazee uliifanya nira yako kuwa nzito sana.


Wana wako wamezimia, Wamelala penye pembe za njia kuu zote Kama kulungu wavuni; Wamejaa hasira ya BWANA, Lawama ya Mungu wako.


nami nitalitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake.


Maana BWANA asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha.


Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadneza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake.


Wamesikia kwamba napiga kite; Hakuna hata mmoja wa kunifariji; Adui zangu wote wamesikia habari ya mashaka yaliyonipata; Hufurahi kwa kuwa umeyafanya hayo; Utaileta siku ile uliyoitangaza, Nao watakuwa kama mimi.


Ameikata pembe yote ya Israeli Katika hasira yake kali; Ameurudisha nyuma mkono wake wa kulia Mbele ya hao adui, Naye amemteketeza Yakobo kama moto uwakao, Ulao pande zote.


Lakini nilitenda kwa ajili ya jina langu, lisitiwe unajisi machoni pa mataifa, ambao niliwatoa mbele ya macho yao.


Lakini nilitenda kwa ajili ya jina langu, ili lisitiwe unajisi mbele ya macho ya mataifa, ambao walikaa pamoja nao, ambao machoni pao nilijidhihirisha kwao, kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.


Na katika siku ile, asema BWANA kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani.


Kwa maana jina la Mungu latukanwa katika Mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa.


Basi hapo walipokuwa karibu na nyumba ya Mika, wakatambua sauti yake huyo kijana Mlawi; ndipo wakageuka wakaenda kuko, na kumwuliza, Je! Ni nani aliyekuleta wewe huku? Unafanya nini mahali hapa? Una kazi gani hapa?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo