Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 52:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Kama vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu),

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Wengi waliomwona walishtuka, kwa vile sura yake ilikuwa imeharibiwa; hakuwa tena na umbo la kibinadamu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Wengi waliomwona walishtuka, kwa vile sura yake ilikuwa imeharibiwa; hakuwa tena na umbo la kibinadamu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Wengi waliomwona walishtuka, kwa vile sura yake ilikuwa imeharibiwa; hakuwa tena na umbo la kibinadamu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kama walivyokuwa wengi walioshangazwa naye, kwani uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote na umbo lake kuharibiwa zaidi ya mfano wa mwanadamu:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kama walivyokuwa wengi walioshangazwa naye, kwani uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote na umbo lake kuharibiwa zaidi ya mfano wa mwanadamu:

Tazama sura Nakili




Isaya 52:14
21 Marejeleo ya Msalaba  

Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti


Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; Wao wananitazama na kunikodolea macho.


Nimekuwa kifani kwa watu wengi, Lakini wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu.


Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.


Ndipo wakamtemea mate usoni, wakampiga ngumi; na wengine wakampiga makofi,


Asimjibu hata neno moja, hata mtawala akastaajabu sana.


Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake;


Nao wakashangaa mno, wakimwambia, Ni nani, basi, awezaye kuokoka?


Nao walikuwako njiani, huku wakipanda kwenda Yerusalemu; na Yesu alikuwa akiwatangulia, wakashangaa, nao katika kufuata wakaogopa. Akawatwaa tena wale Kumi na Wawili, akaanza kuwaambia kuhusu mambo yatakayompata,


Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu.


Akapanda mle katika mashua walimo; upepo ukakoma; wakashangaa sana mioyoni mwao;


wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda mambo yote vema; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme.


Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.


Wakamfunika macho, kisha wakamwulizauliza wakisema, Tabiri, ni nani aliyekupiga?


Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.


Mshangao ukawashika wote, wakamtukuza Mungu; wakajaa hofu, wakisema, Leo tumeona mambo ya ajabu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo