Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 51:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea mkononi mwa BWANA, Kikombe cha hasira yake; Ukalinywea na kumaliza bakuli la kulevyalevya Umelinywea na kulimaliza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Amka ewe Yerusalemu! Amka usimame wima! Mwenyezi-Mungu amekunywesha kikombe cha ghadhabu yake, nawe umeinywa mpaka tone la mwisho, mpaka ukayumbayumba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Amka ewe Yerusalemu! Amka usimame wima! Mwenyezi-Mungu amekunywesha kikombe cha ghadhabu yake, nawe umeinywa mpaka tone la mwisho, mpaka ukayumbayumba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Amka ewe Yerusalemu! Amka usimame wima! Mwenyezi-Mungu amekunywesha kikombe cha ghadhabu yake, nawe umeinywa mpaka tone la mwisho, mpaka ukayumbayumba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Amka, amka! Simama, ee Yerusalemu, wewe uliyekunywa kutoka mkono wa Mwenyezi Mungu kikombe cha ghadhabu yake, wewe uliyekunywa hata machujo yake, kikombe kile cha kunywea kiwafanyacho watu kuyumbayumba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Amka, amka! Simama, ee Yerusalemu, wewe uliyekunywa kutoka mkono wa bwana kikombe cha ghadhabu yake, wewe uliyekunywa mpaka kufikia machujo yake, kikombe kile cha kunywea kiwafanyacho watu kuyumbayumba.

Tazama sura Nakili




Isaya 51:17
30 Marejeleo ya Msalaba  

Macho yake mwenyewe na yaone uharibifu wake, Akanywe ghadhabu zake Mwenyezi.


Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.


Umewaonesha watu wako mazito, Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.


Ili wapenzi wako waopolewe, Utuokoe kwa mkono wako wa kulia, utuitikie.


Nguvu zote za wasio haki nitazimaliza, Lakini nguvu za mwenye haki nitaziimarisha.


Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.


Ngojeni mstaajabu; fanyeni anasa zenu na kuwa vipofu; wamelewa wala si kwa mvinyo; wamewayawaya wala si kwa sababu ya kileo.


Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.


Basi, kwa sababu ya hayo, ulisikilize neno hili, ewe uliyeteswa, na kulewa, lakini si kwa mvinyo;


BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena;


Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.


Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.


Nikayakanyaga makabila ya watu kwa hasira yangu, Nikawalevya kwa ghadhabu yangu, Nami nikaimwaga damu yao chini.


Ndipo utakapowaambia, BWANA asema hivi, Tazama, nitawajaza ulevi wenyeji wote wa nchi hii, hata wafalme wanaoketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na makuhani, na manabii, na wenyeji wote wa Yerusalemu.


yaani, Yerusalemu, na miji ya Yuda, na wafalme wake, na wakuu wake, ili kuwafanya kuwa ukiwa, na ajabu, na mazomeo, na laana; vile vile kama ilivyo leo;


Nawe utawaambia hivi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoutuma kati yenu.


Kwa sababu hiyo ghadhabu yangu, na hasira yangu, zilimwagika, nazo ziliwaka katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, na miji hiyo imeachwa ukiwa, na kuharibika, kama ilivyo leo.


Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbayumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.


Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza.


Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.


Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza.


BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;


hata uwe mwenye wazimu kwa yaonwayo na macho yako, utakayoyaona.


yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-kondoo.


Na mji ule mkuu ukagawanyika katika mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.


Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni mara mbili.


Amka, amka, Debora; Amka, amka, imba wimbo. Inuka, Baraka, wachukue mateka wao Waliokuchukua mateka, Ee mwana wa Abinoamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo