Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 5:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

28 Mishale yao ni mikali, na pinde zao zote zimepindika; Kwato za farasi wao zitahesabika kama gumegume; Na gurudumu zao kama kisulisuli;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Mishale yao ni mikali sana, pinde zao zimevutwa tayari. Kwato za farasi wao ni ngumu kama mawe; mwendo wa magurudumu ya magari ni kimbunga.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Mishale yao ni mikali sana, pinde zao zimevutwa tayari. Kwato za farasi wao ni ngumu kama mawe; mwendo wa magurudumu ya magari ni kimbunga.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Mishale yao ni mikali sana, pinde zao zimevutwa tayari. Kwato za farasi wao ni ngumu kama mawe; mwendo wa magurudumu ya magari ni kimbunga.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Mishale yao ni mikali, pinde zao zote zimevutwa, kwato za farasi wao ziko kama gumegume, magurudumu ya magari yao ya vita ni kama upepo wa kisulisuli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Mishale yao ni mikali, pinde zao zote zimevutwa, kwato za farasi wao ziko kama jiwe la gumegume, magurudumu ya magari yao ya vita ni kama upepo wa kisulisuli.

Tazama sura Nakili




Isaya 5:28
17 Marejeleo ya Msalaba  

Mishale ya mtu hodari iliyochongoka, Pamoja na makaa ya mretemu.


Mishale yako ni mikali, katika mioyo ya adui za mfalme; Watu huanguka chini yako.


Na nyuta zao zitawaangusha vijana; wala hawatahurumia mazao ya tumbo; jicho lao halitawahurumia watoto.


Ufunuo juu ya nyika kando ya bahari. Kama tufani za Negebu zikaribiavyo kwa kasi, inakuja kutoka kwa nyika, toka nchi itishayo.


Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.


Tazama atapanda juu kama mawingu, na magari yake ya vita yatakuwa kama kisulisuli; farasi wake ni wepesi kuliko tai. Ole wetu, kwa sababu tumeharibika.


Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;


Podo lao ni kaburi wazi, ni mashujaa wote pia.


Kwa kwato za farasi wake atazikanyaga njia zako zote; atawaua watu wako kwa upanga, na minara ya nguvu zako itashuka hata nchi.


Nawe utapaa juu, utakuja kama tufani, utakuwa kama wingu kuifunika nchi, wewe, na vikosi vyako vyote, na kabila nyingi za watu pamoja nawe.


Na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati.


Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utapondaponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa BWANA, na mali zao kwa BWANA wa dunia yote.


Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kuparapara, na magari ya vita yenye kurukaruka;


Kisha, kwa kishindo kwato za farasi zilipigapiga, Kwa maana walivyoenda shoti, Walipowakimbiza farasi wenye nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo