Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 45:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Semeni wazi na kutoa hoja zenu; shaurianeni pamoja! Ni nani aliyetangaza zamani matukio ya sasa? Ni nani aliyetamka mambo haya zamani? Je, haikuwa mimi Mwenyezi-Mungu? Hakuna Mungu mwingine ila mimi! Mimi ni Mungu wa haki na mwokozi; hakuna mwingine ila mimi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Semeni wazi na kutoa hoja zenu; shaurianeni pamoja! Ni nani aliyetangaza zamani matukio ya sasa? Ni nani aliyetamka mambo haya zamani? Je, haikuwa mimi Mwenyezi-Mungu? Hakuna Mungu mwingine ila mimi! Mimi ni Mungu wa haki na mwokozi; hakuna mwingine ila mimi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Semeni wazi na kutoa hoja zenu; shaurianeni pamoja! Ni nani aliyetangaza zamani matukio ya sasa? Ni nani aliyetamka mambo haya zamani? Je, haikuwa mimi Mwenyezi-Mungu? Hakuna Mungu mwingine ila mimi! Mimi ni Mungu wa haki na mwokozi; hakuna mwingine ila mimi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Tangazeni litakalokuwepo, lisemeni hilo; wao na wafanye shauri pamoja. Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani, aliyelitangaza tangu zamani za kale? Je, haikuwa Mimi, Mwenyezi Mungu? Wala hapana Mungu mwingine zaidi yangu mimi, Mungu mwenye haki na Mwokozi; hapana mwingine ila mimi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Tangazeni litakalokuwepo, lisemeni hilo, wao na wafanye shauri pamoja. Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani, aliyetangaza tangu zamani za kale? Je, haikuwa Mimi, bwana? Wala hapana Mungu mwingine zaidi yangu mimi, Mungu mwenye haki na Mwokozi; hapana mwingine ila mimi.

Tazama sura Nakili




Isaya 45:21
33 Marejeleo ya Msalaba  

Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu.


Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye Juu, juu ya nchi yote.


Semeni katika mataifa, BWANA ametamalaki; Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike, Atawahukumu watu kwa adili.


Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia BWANA kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi wa kuwatetea, naye atawaokoa.


Ni nani aliyeihubiri habari tokea mwanzo, tupate kuijua? Na tokea zamani, tupate kusema, Yeye ni mwenye haki? Naam, hapana hata mmoja aliyetujulisha; naam, hapana hata mmoja aliyetuonesha; naam, hapana hata mmoja aliyesikia maneno yenu.


Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi.


Maana mimi ni BWANA, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako.


Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli.


BWANA asema hivi, Kazi ya Misri, na bidhaa ya Kushi, na Waseba, watu walio warefu, watakujia, nao watakuwa wako; watakufuata; watakuja katika minyororo; wataanguka chini mbele yako, watakuomba, wakisema, Hakika Mungu yu ndani yako; wala hapana mwingine, hapana Mungu tena.


Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba iwe ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.


Katika BWANA wazao wote wa Israeli watapewa haki, na kutukuka.


Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakuimarisha ijapokuwa hukunijua;


Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? BWANA amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo.


Mimi nimehubiri mambo ya kale tangu zamani; naam, yalitoka katika kinywa changu, nikayadhihirisha; niliyatenda kwa ghafla, yakatokea.


Utanyonya maziwa ya mataifa, Utanyonya matiti ya wafalme; Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, Na mkombozi wako, Mwenye enzi wa Yakobo.


Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.


Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.


Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu nchi ya Misri; wala hutamjua mungu mwingine ila mimi; wala zaidi ya mimi hakuna mwokozi.


BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.


BWANA kati yake ni mwenye haki; hatatenda uovu; kila asubuhi hudhihirisha hukumu yake, wala hakomi; bali mtu asiye haki hajui kuona haya.


lakini itakuwa siku moja, iliyojulikana na BWANA; si mchana, wala si usiku; lakini itakuwa, ya kwamba wakati wa jioni kutakuwako nuru.


Naye BWANA atakuwa Mfalme wa nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja.


Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.


Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo