Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 44:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 niviambiaye vilindi, Kauka, nami nitaikausha mito yako;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Mimi ndimi ninayeviamuru vilindi: Kaukeni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Mimi ndimi ninayeviamuru vilindi: Kaukeni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Mimi ndimi ninayeviamuru vilindi: Kaukeni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 niiambiaye kilindi cha maji, ‘Kauka, nami nitakausha vijito vyako,’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 niambiaye kilindi cha maji, ‘Kauka, nami nitakausha vijito vyako,’

Tazama sura Nakili




Isaya 44:27
14 Marejeleo ya Msalaba  

Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;


Wewe ulitokeza chemchemi na kijito; Wewe ulikausha mito yenye maji sikuzote.


Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika.


Nitaharibu milima na vilima, nitavikausha vyote vimeavyo; nitaifanya mito ya maji kuwa visiwa, na kuyakausha maziwa ya maji.


BWANA asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu;


Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.


Maana mimi ni BWANA, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake yakavuma.


Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu, kwa mkono wa kulia wa Musa? Aliyeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele?


Ukosefu wa mvua uko juu ya maji yake, nayo yatakaushwa; maana ni nchi ya sanamu za kuchongwa, nao wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu.


Navyo vivuko vimeshambuliwa, Nayo makangaga wameyatia moto, Nao watu wa vita wameingiwa na hofu.


Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu.


Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto Nile vitakauka; na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka.


Na huyo wa sita akalimimina bakuli lake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo