Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 42:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang'anyi? Si yeye, BWANA? Yeye tuliyemkosea, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Ni nani aliyewatia Waisraeli mikononi mwa adui zao? Nani aliyewaacha wanyanganywe mali zao? Ni Mwenyezi-Mungu ambaye tumemkosea! Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake, wala hawakuzitii amri zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Ni nani aliyewatia Waisraeli mikononi mwa adui zao? Nani aliyewaacha wanyanganywe mali zao? Ni Mwenyezi-Mungu ambaye tumemkosea! Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake, wala hawakuzitii amri zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Ni nani aliyewatia Waisraeli mikononi mwa adui zao? Nani aliyewaacha wanyang'anywe mali zao? Ni Mwenyezi-Mungu ambaye tumemkosea! Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake, wala hawakuzitii amri zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka, na Israeli kwa wateka nyara? Je, hakuwa yeye, Mwenyezi Mungu, ambaye tumetenda dhambi dhidi yake? Kwa kuwa hawakufuata njia zake, hawakutii sheria zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka, na Israeli kwa wateka nyara? Je, hakuwa yeye, bwana, ambaye tumetenda dhambi dhidi yake? Kwa kuwa hawakufuata njia zake, hawakutii sheria zake.

Tazama sura Nakili




Isaya 42:24
29 Marejeleo ya Msalaba  

Walivunjikavunjika, taifa juu ya taifa, na mji juu ya mji; kwa sababu Mungu aliwafadhaisha kwa shida zote.


Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mnyonge; akawatia wote mkononi mwake.


Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao, Waenende katika mashauri yao.


Laiti watu wangu wangenisikiliza, Na Israeli angeenenda katika njia zangu;


Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali.


Ni nani miongoni mwenu atakayetega sikio lake kuyasikia hayo? Atakayesikiliza na kusikia kwa wakati ujao?


Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.


Nilikuwa nimekasirika na watu wangu, niliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; kwa wazee uliifanya nira yako kuwa nzito sana.


Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;


Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake niliona hasira, nikampiga; nilificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe.


Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.


Hawajanyenyekea hata leo, wala hawakuogopa, wala hawakuenenda katika sheria yangu, wala katika amri zangu, nilizoweka mbele yenu, na mbele ya baba zenu.


Angalia, nitaleta taifa juu yenu litokalo mbali sana, Ee nyumba ya Israeli, asema BWANA; ni taifa hodari, ni taifa la zamani sana, taifa ambalo hujui lugha yake, wala huyafahamu wasemayo.


Kongwa la makosa yangu limefungwa na mkono wake; Hayo yameshikamana; Yamepanda juu shingoni mwangu; Amezikomesha nguvu zangu;


BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.


Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake.


Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?


Basi yule mfalme akaghadhibika; akatuma majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.


BWANA atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake;


Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama BWANA asingaliwatoa?


Hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, akawauza na kuwaua mikononi mwa Wafilisti, na mikononi mwa wana wa Amoni.


Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.


Kwa hiyo hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, naye akawauza na kuwatia mikononi mwa Kushan-rishathaimu mfalme wa Mesopotamia; na wana wa Israeli wakamtumikia huyo Kushan-rishathaimu muda wa miaka minane.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo