Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 42:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa BWANA?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Nani aliye kipofu ila mtumishi wangu? Nani aliye kiziwi kama mjumbe ninayemtuma? Ni nani aliye kipofu kama huyu niliyemweka wakfu, au kipofu kama mtumishi wa Mwenyezi-Mungu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Nani aliye kipofu ila mtumishi wangu? Nani aliye kiziwi kama mjumbe ninayemtuma? Ni nani aliye kipofu kama huyu niliyemweka wakfu, au kipofu kama mtumishi wa Mwenyezi-Mungu?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Nani aliye kipofu ila mtumishi wangu? Nani aliye kiziwi kama mjumbe ninayemtuma? Ni nani aliye kipofu kama huyu niliyemweka wakfu, au kipofu kama mtumishi wa Mwenyezi-Mungu?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Ni nani aliye kipofu isipokuwa mtumishi wangu, na kiziwi kama mjumbe ninayemtuma? Ni nani aliye kipofu kama yeye aliyejitoa kwangu, aliye kipofu kama mtumishi wa Mwenyezi Mungu?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Ni nani aliye kipofu isipokuwa mtumishi wangu, na kiziwi kama mjumbe ninayemtuma? Ni nani aliye kipofu kama yeye aliyejitoa kwangu, aliye kipofu kama mtumishi wa bwana?

Tazama sura Nakili




Isaya 42:19
26 Marejeleo ya Msalaba  

Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.


Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami.


Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho kitabu, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.


Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Abrahamu, rafiki yangu;


Walete watu wasioona, japo wana macho, wasiosikia japo wana masikio.


nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka;


Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.


Naye akaniambia, Nenda, ukawaambie watu hawa, Endeleeni kusikia, lakini msifahamu; endeleeni kutazama, lakini msione.


Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa.


Sikilizeni neno hili, enyi watu wajinga msio na ufahamu; mlio na macho ila hamuoni; mlio na masikio ila hamsikii.


Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.


Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.


Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.


Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.


Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini kwa kuwa sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.


Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.


ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, wasiione nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo