Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Isaya 37:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 Maana katika Yerusalemu yatatoka mabaki, nao watakaookoka katika mlima Sayuni; wivu wa BWANA wa majeshi utatimiza mambo hayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Maana kutakuwa na watu watakaosalia huko Yerusalemu; naam, huko mlimani Siyoni kutakuwako watu wachache watakaosalimika.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi amedhamiria kukamilisha hayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Maana kutakuwa na watu watakaosalia huko Yerusalemu; naam, huko mlimani Siyoni kutakuwako watu wachache watakaosalimika.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi amedhamiria kukamilisha hayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Maana kutakuwa na watu watakaosalia huko Yerusalemu; naam, huko mlimani Siyoni kutakuwako watu wachache watakaosalimika.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi amedhamiria kukamilisha hayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Kwa kuwa kutoka Yerusalemu watakuja mabaki, na kutoka Mlima Sayuni kundi la walionusurika. Wivu wa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, ndio utatimiza jambo hili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Kwa kuwa kutoka Yerusalemu watakuja mabaki, na kutoka Mlima Sayuni kundi la walionusurika. Wivu wa bwana Mwenye Nguvu Zote, ndio utatimiza jambo hili.

Tazama sura Nakili




Isaya 37:32
13 Marejeleo ya Msalaba  

Maana mabaki yatatoka katika Yerusalemu, na wao watakaookoka katika mlima wa Sayuni wivu wa BWANA utatimiza jambo hilo.


Tena itakuwa katika siku hiyo mabaki ya Israeli, na hao waliopona wa nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga, bali watamtegemea BWANA, Mtakatifu wa Israeli, kwa kweli.


BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.


Basi sasa, BWANA, Mungu wetu, utuokoe kutoka kwa mkono wake, falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe BWANA, wewe peke yako.


Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno ya huyo kamanda ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; na BWANA, Mungu wako atayakemea maneno aliyoyasikia; basi, inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.


Siku hiyo chipukizi la BWANA litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.


BWANA atatokea kama shujaa; Ataamsha wivu kama mtu wa vita; Atalia, naam, atapiga kelele; Atawatenda adui zake mambo makuu.


Akajivika haki kama deraya kifuani, na chapeo cha wokovu kichwani pake, akajivika mavazi ya kisasi yawe mavazi yake, naye alivikwa wivu kama joho.


Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.


Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.


Mamlaka ya enzi yake yatakuzwa daima, Na kutakuwa na amani isiyo na mwisho, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.


Hapo ndipo BWANA alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake, akawahurumia watu wake.


Basi yule malaika aliyesema nami akaniambia, Haya, piga kelele na kusema, BWANA wa majeshi asema hivi, Naona wivu kwa ajili ya Yerusalemu, na kwa ajili ya Sayuni; naona wivu mkuu sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo