Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Isaya 37:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Ndiyo sababu wenyeji wao wakawa hawana nguvu, na kufadhaika, na kuhangaika, wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya madari, kama shamba la ngano kabla haijaiva.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu, wametishika na kufadhaika. Wamekuwa kama mimea shambani, kama nyasi changa shambani, kama majani yaotayo juu ya paa au kama ngano kabla hazijakomaa ambazo hunyauka upepo mkavu uvumapo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu, wametishika na kufadhaika. Wamekuwa kama mimea shambani, kama nyasi changa shambani, kama majani yaotayo juu ya paa au kama ngano kabla hazijakomaa ambazo hunyauka upepo mkavu uvumapo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu, wametishika na kufadhaika. Wamekuwa kama mimea shambani, kama nyasi changa shambani, kama majani yaotayo juu ya paa au kama ngano kabla hazijakomaa ambazo hunyauka upepo mkavu uvumapo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu, wanavunjika mioyo na kuaibishwa. Wao ni kama mimea katika shamba, kama machipukizi mororo ya kijani, kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba, ambayo hukauka kabla ya kukua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu, wanavunjika mioyo na kuaibishwa. Wao ni kama mimea katika shamba, kama machipukizi mororo ya kijani, kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba, ambayo hukauka kabla ya kukua.

Tazama sura Nakili

Isaya 37:27
17 Marejeleo ya Msalaba  

Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao.

Ndiyo sababu wenyeji wao walikuwa na nguvu chache, wakafadhaika, na kuhangaika; wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, na kama ngano iliyokaushwa kabla haijaiva.

Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo anavyostawi.

Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea.

Maana kama majani watakatika mara, Kama miche mibichi watanyauka.

Hata wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakastawi. Mwishowe wataangamizwa milele;

Katika siku hiyo Misri itakuwa kama wanawake; itatetemeka na kuogopa kwa sababu ya kutikiswa kwa mkono wa BWANA wa majeshi, autikisao juu yake.

Maana mngelipiga jeshi lote la Wakaldayo wanaopigana nanyi, wakabaki kati yao watu waliojeruhiwa tu, hata hivyo wangeondoka kila mtu katika hema yake, na kuuteketeza mji huu.

Pandeni juu ya kuta zake mkaharibu, lakini msiharibu kabisa; ondoeni matawi yake; kwa maana si yake BWANA.

Nanyi mmejitukuza juu yangu kwa vinywa vyenu, na kuyaongeza maneno juu yangu; nimesikia mimi.

Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; kinga iliyokuwa juu yao imeondolewa, naye BWANA yuko pamoja nasi; msiwaogope.

Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba.

Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo