Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 37:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Tega sikio lako, BWANA, usikie; funua macho yako, BWANA, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, aliyopeleka ili kumtukana Mungu aliye hai.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Ee, Mwenyezi-Mungu, fumbua macho uone, tega sikio lako, uyasikie matusi yote ambayo Senakeribu amepeleka na kukutukana wewe Mungu uliye hai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Ee, Mwenyezi-Mungu, fumbua macho uone, tega sikio lako, uyasikie matusi yote ambayo Senakeribu amepeleka na kukutukana wewe Mungu uliye hai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Ee, Mwenyezi-Mungu, fumbua macho uone, tega sikio lako, uyasikie matusi yote ambayo Senakeribu amepeleka na kukutukana wewe Mungu uliye hai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Tega sikio, Ee Mwenyezi Mungu, usikie; fungua macho yako, Ee Mwenyezi Mungu, uone; sikiliza maneno yote ambayo Senakeribu ametuma kumtukana Mungu aliye hai.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Tega sikio, Ee bwana, usikie; fungua macho yako, Ee bwana, uone; sikiliza maneno yote ambayo Senakeribu ametuma kumtukana Mungu aliye hai.

Tazama sura Nakili




Isaya 37:17
17 Marejeleo ya Msalaba  

Labda BWANA atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye BWANA atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo.


Tega sikio lako, Ee BWANA, usikie; fumbua macho yako, Ee BWANA, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, ambayo amemtuma mtu aje nayo ili kumtukana Mungu aliye hai.


Na sasa, Ee Mungu wangu, macho yako yafumbuke, nakusihi, masikio yako yakasikilize maombi yaombwayo mahali hapa.


Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.


Yeye hawaondolei macho yake wenye haki; Lakini pamoja na wafalme huwaweka Katika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.


Haleluya. Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu.


Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, Utege sikio lako ulisikie neno langu.


Kwa haki yako uniponye, uniponye, Unitegee sikio lako, uniokoe.


Ee Mungu, mtesi atalaumu hata lini? Adui alidharau jina lako hata milele?


Ee Mungu, usimame, ujitetee mwenyewe, Ukumbuke unavyotukanwa na mpumbavu mchana kutwa.


Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao Laumu zao walizokulaumu, Ee Bwana.


Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno ya huyo kamanda ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; na BWANA, Mungu wako atayakemea maneno aliyoyasikia; basi, inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.


Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana uko juu ya watenda mabaya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo