Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Isaya 36:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 wala msimwache Hezekia kuwatia moyo wa kumtumaini BWANA; akisema, BWANA bila shaka atatuokoa, mji huu hautatiwa katika mkono wa mfalme wa Ashuru.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Msikubali awashawishi ili mumtegemee Mwenyezi-Mungu akisema, ‘Mwenyezi-Mungu hakika atatuokoa na mji huu hautatiwa mkononi mwa mfalme wa Ashuru.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Msikubali awashawishi ili mumtegemee Mwenyezi-Mungu akisema, ‘Mwenyezi-Mungu hakika atatuokoa na mji huu hautatiwa mkononi mwa mfalme wa Ashuru.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Msikubali awashawishi ili mumtegemee Mwenyezi-Mungu akisema, ‘Mwenyezi-Mungu hakika atatuokoa na mji huu hautatiwa mkononi mwa mfalme wa Ashuru.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Msikubali Hezekia awashawishi kumtumaini Mwenyezi Mungu kwa kuwaambia, ‘Hakika Mwenyezi Mungu atatuokoa. Mji huu hautaangukia mikononi mwa mfalme wa Ashuru.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Msikubali Hezekia awashawishi kumtumaini bwana kwa kuwaambia, ‘Hakika bwana atatuokoa. Mji huu hautaangukia mikononi mwa mfalme wa Ashuru.’

Tazama sura Nakili




Isaya 36:15
10 Marejeleo ya Msalaba  

Enyi wanadamu, hadi lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo hadi lini?


Jihadharini, Hezekia asije akawadanganya, akisema, BWANA atatuokoa. Je! Kati ya miungu ya mataifa, kuna yeyote aliyewahi kuokoa nchi yake kutoka kwa mkono wa mfalme wa Ashuru?


Katika miungu yote ya nchi hizi ni nani waliookoa nchi yao kutoka kwa mkono wangu, hata BWANA auokoe Yerusalemu kutoka kwa mkono wangu?


Lakini ukiniambia, Tunamtumaini BWANA, Mungu wetu, je! Si yeye ambaye Hezekia ameondoa mahali pake mlimoinuka, na madhabahu zake, akawaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, Sujuduni mbele ya madhabahu hii?


Mwambieni Hezekia, mfalme wa Yuda, maneno haya, mkisema, Asikudanganye Mungu wako unayemtumaini, akisema, Yerusalemu hautatiwa katika mikono ya mfalme wa Ashuru.


Tazama, umesikia habari ya mambo yote, ambayo wafalme wa Ashuru wamezitenda nchi zote, kwa kuziangamiza kabisa je! Utaokoka wewe?


Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo