Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 33:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Bali huko BWANA atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Humo Mwenyezi-Mungu atatuonesha ukuu wake. Kutakuwa na mito mikubwa na vijito, ambamo meli za vita hazitapita, wala meli kubwa kuingia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Humo Mwenyezi-Mungu atatuonesha ukuu wake. Kutakuwa na mito mikubwa na vijito, ambamo meli za vita hazitapita, wala meli kubwa kuingia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Humo Mwenyezi-Mungu atatuonesha ukuu wake. Kutakuwa na mito mikubwa na vijito, ambamo meli za vita hazitapita, wala meli kubwa kuingia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Huko Mwenyezi Mungu atakuwa Mwenye Nguvu wetu. Patakuwa kama mahali pa mito mipana na vijito. Hakuna jahazi lenye makasia litakalopita huko, wala hakuna meli yenye nguvu itakayopita huko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Huko bwana atakuwa Mwenye Nguvu wetu. Patakuwa kama mahali pa mito mipana na vijito. Hakuna jahazi lenye makasia litakalopita huko, wala hakuna meli yenye nguvu itakayopita huko.

Tazama sura Nakili




Isaya 33:21
14 Marejeleo ya Msalaba  

Sauti ya BWANA inasikika juu ya maji; Mungu wa utukufu apiga radi; BWANA yu juu ya maji mengi.


Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.


Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri wake, yataona nchi iliyoenea sana.


Nitafunua vijito vya maji juu ya vilima, na chemchemi katikati ya mabonde; nitageuza jangwa kuwa ziwa la maji, na mahali pakavu kuwa vijito vya maji.


Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.


Wanyama pori wataniheshimu, mbweha pia na mbuni; kwa sababu nimewapa maji jangwani, na mito nyikani, ili kuwanywesha watu wangu, wateule wangu;


Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;


Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa.


Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka ya hao waliowatumikia; nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma.


Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. BWANA, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme iko katikati yao.


Naye akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Harani,


Usimrudishe kwa bwana wake mtumwa aliyejiponya kutoka kwa bwana wake kuja kwako;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo