Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 33:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri wake, yataona nchi iliyoenea sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Mtaweza kumwona mfalme katika fahari yake, mtaiona nchi anayotawala, kubwa na pana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Mtaweza kumwona mfalme katika fahari yake, mtaiona nchi anayotawala, kubwa na pana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Mtaweza kumwona mfalme katika fahari yake, mtaiona nchi anayotawala, kubwa na pana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake na kuiona nchi inayoenea mbali.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake na kuiona nchi inayoenea mbali.

Tazama sura Nakili




Isaya 33:17
20 Marejeleo ya Msalaba  

Watu wengi walimletea BWANA zawadi huko Yerusalemu, na vitu vya thamani kwa Hezekia, mfalme wa Yuda; hata yeye akatukuka tangu wakati ule machoni pa mataifa yote.


Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu!


Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha mahali penye usalama.


Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu; Neema imemiminiwa midomoni mwako, Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.


Mpendwa wangu ni mweupe, tena mwekundu, Mashuhuri miongoni mwa elfu kumi;


Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa BWANA wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.


Umeliongeza hilo taifa, BWANA, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.


Bali huko BWANA atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo.


Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.


Ikawa mfalme Hezekia aliposikia hayo, alizirarua nguo zake, akajivika nguo za magunia, akaingia katika nyumba ya BWANA.


Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.


Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi! Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi! Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake.


akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.


Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.


Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.


Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.


tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.


Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini tunajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo